Naibu
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Tulia Akson
akiongoza Mbio za Tulia Marathon KM 5 zilizofanyika jana asubuhi kuanzia
Bungeni Mpaka Nyerere Square zikishirikishwa wabunge mbalimbali wakuu
wa wilaya na vijana kama juhudi za kuunga mkono Juhudi za Rais John
Pombe Magufuli katika kuwaletea wananchi maendeleo nchini kushoto ni
Anthony Mtaka Rais wa Chama cha Riadha Nchini RT.
Baada ya
mbio hizo walikwenda kutoa msaada wa vitu mbalimbali katika kituo cha
Watoto Yatima kiitwacho kijiji cha Matumaini kilichopo nje kidogo ya mji
wa Dodoma.Wakati wa kutoa msaada huo Dkt Tulia alisema kuwa ni vvema
kila Mkoa ukawa na vikundi mbalimbali kikiwemo cha Wazalendo wakafanya
shughuli za Kijamii kusaidia makundi mbalimbali
Naibu
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Tulia Akson akiwa
na Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde Rais wa
Chama Cha Riadha Tanzania RT Bw. Anthony Mtaka , Mbunge wa Viti Maalum
mkoa wa Mbeya Mary Majelwa wakishiriki katika mbio hizo jana asubuhi.
Naibu
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Tulia Akson
akipiga makofi kama ishara ya kushukuru mara baada ya kufika mwisho wa
mbio hizo zilizoishia Nyerere Square , kushoto ni Naibu Waziri wa Kazi,
Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde.
Vijana wakipasha mara baada ya kufika kwenye viwanja vya Nyerere Squre.
Mkuu wa
mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda kulia na Mbunge wa jimbo la
Chalinze wa pili kushoto wakishiriki katika mbio hizo pamoja na vijana
mbalimbali .(P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment