Donald Trump akisalimiana na mgombea mwenza wake Mike Pence
Donald
Trump ameahidi kukomesha matukio ya uhalifu na vurugu nchini Marekani
endapo atafanikiwa kuwa rais mteule wa taifa hilo, ahadi hii ameitoa
kwatika hotuba yake wakati alipokuwa anathibitisha ukubalifu wake wa
kuteuliwa kuwa mgombea urais kwa tiketi ya chama cha Republican.
Maneno
ama ahadi hiyo imo katika moja ya kifungu cha hotuba yake hii ni baada
ya kuvuja kwa hotuba hiyo na kudakuliwa na wataalamu wa udakuzi na
kueleza kuwa hotuba hiyo imesheheni ahadi tele za ya kurejesha utawala
wa sheria , ikiwemo suala la kukabiliana na uhamiaji haramu na kwamba
suala hilo ataliingiza katika sera za kigeni za Marekani.
Pamoja na
hayo Trump anatarajiwa kutoa tamko kuwa mara moja atahakikisha
anasimamia suala la wahamiaji haramu kutokana na mataifa kuathiriwa na
wimbi la masuala ya ugaidi na kusisitiza ahadi yake ya kujenga ukuta
kwenye mpaka baina ya Marekani n a nchi ya Mexico ili kuondokana na
suala la wahamiaji.
Naye
mpinzani wa Donald Trump bibi Hillary Clinton, atathibitishwa juma
lijalo kupitia chama chake cha Democrats ambapo chama hicho kitakuwa
mkutano mkubwa katika jimbo la Philadelphia.BBC
SHARE
No comments:
Post a Comment