Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani (wa kwanza kulia)
akizungumza na Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo, Massana
Mwishawa (wa pili kulia) alipotembelea hifadhi hiyo tarehe 21 Julai,
2016 kwa ajili ya kujionea kero mbalimbali na kuzitafutia ufumbuzi.
Kushoto aliyesimama na Mbunge wa Jimbo la Geita Vijijini, Joseph Kasheku
maarufu kwa jina la Msukuma.
Mkuu wa
Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo, Massana Mwishawa (wa pili kulia)
akimuonesha Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani (wa
kwanza kulia) sehemu ya fukwe za hifadhi hiyo ambazo ni makazi ya Mamba
na Ndege wa aina mbali mbali alipotembelea hifadhi hiyo tarehe 21 Julai,
2016 kwa ajili ya kujionea kero mbalimbali na kuzitafutia ufumbuzi.
Kushoto aliyesimama na Mbunge wa Jimbo la Geita Vijijini, Joseph Kasheku
maarufu kwa jina la Msukuma.
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani (wa pili kulia) akiteta
jambo na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mwl. Herman Kapufi (kulia) katika
fukwe ya Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo alipotembelea hifadhi
hiyo tarehe 21 Julai, 2016 kwa ajili ya kujionea kero mbalimbali na
kuzitafutia ufumbuzi. Kushoto anaesaini kitabu cha wageni ni Mbunge wa
Jimbo la Geita Vijijini, Joseph Kasheku maarufu kwa jina la Msukuma.
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani (katikati waliokaa),
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mwl. Herman Kapufi (wa tatu kushoto
waliokaa), Mbunge wa Jimbo la Geita Vijijini, Joseph Kasheku maarufu kwa
jina la Msukuma (wa tatu kulia waliokaa), Kaimu Mkurugenzi Mkuu TANAPA,
Ibrahim Mussa (wa pili kushoto waliokaa) na baadhi ya Watumishi wa
Hifadhi ya Taifa Kisiwa cha Rubondo hifadhini hapo tarehe 21 Julai,
2016.
NA HAMZA TEMBA – WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani ameitaka Mamlaka ya
Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kuzishirikisha jamii zinazozunguka
maeneo ya hifadhi hapa nchini kutambua umuhimu wa kuhifadhi maeneo hayo
ili kutoa ulinzi shirikishi katika kupambana na Ujangili.
Eng.
Makani amesema hayo jana wakati akizungumza na viongozi pamoja na
watumishi wa Mamlaka hiyo akiwa ziarani Mkoani Geita katika Hifadhi ya
Taifa ya Kisiwa cha Rubondo.
“Wananchi
waoishi jirani na maeneo haya ya hifadhi ni muhimu wakaelimishwa juu ya
faida za uhifadhi kiikolojia na kiuchumi kwenye maisha yao ambapo
itawapa msukumo wa kuyatunza na kuyalinda” Alisema Eng. Makani.
Aliongeza
kuwa vita dhidi ya Ujangili hapa nchini haiwezi kufanikiwa kirahisi
iwapo jamii inayozunguka maeneo ya Hifadhi haitatoa ushirikiano kwa
Serikali katika kulinda na kuhifadhi Maliasili zilizopo.
“Pamoja
na mbinu nyingine, washirikisheni wananchi watusaidie kupambana na
ujangili ili fedha ambayo ingetumiwa na Serikali kwa kazi hiyo itumike
kuendeleza hifadhi zetu pamoja na kutoa huduma nyingine za kijamii”
Alisema Eng. Makani.
Akizungumzia
faida za uhifadhi kiuchumi hapa nchini alisema kuwa, Sekta ya utalii
ndio sekta pekee inayoongoza kwa kuliingizia taifa mapato mengi ya nje
(foreign currency) ambayo ni asilimia 25 ya mapato yote. Sekta hiyo pia
inachangia pato la taifa kwa asilimia 17.2.
Eng.
Makani aliongeza kuwa “Serikali ya awamu ya tano ina mpango wa kuboresha
sekta ya utalii ili iweze kuiingizia zaidi mapato, katika kufanikisha
hilo tumeweka mkakati wa kuboresha ofisi zetu za utalii za Kanda ili
ziweze kutangaza na kukuza zaidi utalii wa ndani”.
Kwa
upande wa hoteli zinazotoa huduma ya kitalii hapa nchini alisema kuwa
ifikapo mwezi Septemba mwaka huu, Serikali itaanza rasmi zoezi la
kuorodhesha hoteli zote zinazotoa huduma hiyo na kuzipanga kwenye
makundi ya ubora ambapo zile zitakazoonekana hazina hadhi kabisa
zitaondolewa katika mtandao wa kutoa huduma hiyo. Alisema zoezi hilo
litaboresha huduma za kitalii nchini na kusaidia watalii kufikia hoteli
wanazozihitaji na kupata huduma stahiki .
Katika
kushirikisha sekta binafsi kwenye kukuza utalii nchini, amewaomba watoa
huduma za ndege kuangalia upya viwango vya gharama zao za usafiri ili
wananchi wengi zaidi waweze kumudu na kunufaika na huduma hiyo.
Wakati huo huo aliwaasa watumishi wa Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo kufanya kazi kwa bidii, kuwa na maadili
mema na uadilifu kazini. Aliwataka pia kuwa mstari wa mbele kupiga vita ujangili, kuboresha ukusanyaji wa mapato na kushirikisha wananchi kwenye uhifadhi.
mema na uadilifu kazini. Aliwataka pia kuwa mstari wa mbele kupiga vita ujangili, kuboresha ukusanyaji wa mapato na kushirikisha wananchi kwenye uhifadhi.
Hapo
awali akiwasilisha taarifa ya hifadhi hiyo kwa Naibu Waziri wa
Maliasili, Eng. Ramo Makani, Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha
Rubondo, Massana Mwishawa alisema kuwa changamoto kubwa inayoikabili
hifadhi hiyo ni ujangili na upatikanaji mdogo wa mapato ambao hauwiani
na mahitaji ya hifadhi hiyo.
Kwa
upande wake Mbunge wa Jimbo la Geita Vijijini, Joseph Luiza Kasheku
maarufu kama Msukuma, alimuomba Naibu Waziri huyo wa Maliasili kuboresha
Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo ambayo ipo Jimboni kwake iweze
kupata mapato ya kutosha na kujiendesha yenyewe. Hifadhi hiyo kwa sasa
inategemea mapato kutoka kwenye hifadhi nyingine
kujiendesha.
kujiendesha.
Hifadhi
ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo iliyopo Mkoani Geita ni moja ya sehemu
pekee na muhimu katika uzalishaji wa mazalia ya samaki katika ziwa
Victoria. Sehemu nyingine ni Hifadhi ya Kisiwa cha Saanane iliyopo
Mkoani Mwanza. Hifadhi hizi zina umuhimu mkubwa katika upatikanaji wa
samaki katika Ziwa Victoria.(P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment