Na Leonard Msigwa/GPL
Maelfu ya
wafuasi wa chama tawala cha ZANU-PF nchini Zimbabwe wameandamana kwenye
mji mkuu wa nchi hiyo Harare, kwa lengo la kumuunga mkono Rais Mugabe
aliyetawala nchi hiyo kwa kipindi cha miaka 36.
Maandamano
hayo yamekuja siku chache baada ya mlolongo wa matukio ya wapinzani wa
kiongozi huyo mwenye miaka 92 kumtaka aachie madaraka. Wakilalamikia
kushuka kwa uchumi, rushwa na uvunjifu wa haki za binadamu.
Mgomo
kazini ulioitishwa kupitia mitandao ya kijamii na mchungaji Evan
Mawarire, mapema mwezi huu umepata mwitikio mkubwa nchi nzima kwa mara
ya kwanza katika historia ya nchi hiyo.
Rais
Mugabe jana jumanne alimpinga mchungaji Mawarire kwa uwazi mbele ya
halaiki huku akimtaja jina lake na kumwambia yeye na wafuasi wake
wanaweza kuhama nchini Zimbabwe endapo wanaona hawana furaha kuishi
nchini humo.
Wafuasi hao walikuwa wakiimba nyimbo mbalimbali za kumuunga mkono kiongozi huyo wakiwa na mabango mbalimbali yenye picha zake.(P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment