Naibu
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Angeline Mabula
wakati akikagua nyumba za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Wilayani
Mkinga wengine ni Mkuu wa Wilaya ya Mkinga Yona Maki (mwenye tai) na
Meneja NHC Tanga Issaya Mshamba.
Baadhi ya
Nyumba za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) zilizopo Wilayani Mkinga
ambazo Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt
Angeline Mabula ameamuru watumishi wa wilaya hiyo waamie ifikapo tarehe 1
Agosti 2016.
Naibu
Waziri wa Ardhi Mhe. Dkt Angeline Mabula akiteta jambo na mkuu wa wilaya
ya Handeni Godwin Gondwe (mwenye tai nyekundu) mara baada ya kujadili
changamoto za ardhi katika wilaya hiyo.
Naibu
Waziri wa Ardhi Mhe. Dkt Angeline Mabula akiongea na wananchi wa Hale
wilayani Korogwe mkoani Tanga na kutolea ufumbuzi migogoro ya Ardhi
inayowakabili.
Naibu Waziri wa Ardhi Mhe. Dkt Angeline Mabula akiongea na watumishi wa halmashauri ya manispaa ya Tanga. PICHA ZOTE NA KITENGO CHA MAWASILIANO WIZARA YA ARDHI.
Naibu
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angeline Mabula
ametoa Siku kumi na mbili kwa watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya
Mkinga kuhama Tanga Mjini na kuhamia Wilayani Mkinga mahali zilipo
nyumba za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) zilizojengwa kwa ajili yao.
Naibu
Waziri Mabula ametoa kauli hiyo wakati wa ziara yake wilayani Mkinga
ambapo pamoja na mambo mengine alipata nafasi ya kutembelea eneo
zilipojengwa nyumba hizo na kumuagiza Meneja wa NHC mkoa wa Tanga
kuhakikisha tarehe 1 mwezi wa Agosti 2016 watumishi hao wanahamia katika
nyumba hizo.
kwa
sasa watumishi hao wamekuwa wakiishi Tanga mjini na kufanya kazi
wilayani mkinga, hali inayowalazimu kusafiri zaidi ya kilometa 50
kilasiku kwenda na kurudi.
Mheshimiwa
Mabula yupo katika ziara ya siku nne mkoani Tanga ambapo anatembelea
Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya wilaya za Tanga mjini, Korogwe pamoja na
kuzindua baraza jipya la Wilaya ya Kilindi. Hata hivyo mbali na mabaraza
ya Ardhi mheshimiwa Naibu Waziri anatembelea miradi ya NHC pamoja na
kutatua kero za migogoro ya Ardhi na changamoto za watumishi wa sekta za
Ardhi mkoani Tanga.(P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment