
Mapigano
makali yamezuka Jumapili (10.07.2016) katika mji mkuu wa Sudan Kusini wa
Juba na kupelekea maelfu ya watu kuukimbia mji huo kufuatia siku kadhaa
za mapambano kati ya vikosi vya serikali na waasi
Mapigano
makali yamezuka Jumapili (10.07.2016) katika mji mkuu wa Sudan Kusini wa
Juba na kupelekea maelfu ya watu kuukimbia mji huo kufuatia siku kadhaa
za mapambano kati ya vikosi vya serikali na waasi.
Mashuhuda
wamesema sehemu kubwa ya mapigano hayo yametokea katika kitongoji cha
Jebel ambapo makamo wa rais Riek Machar kiongozi wa waasi hadi hapo
ilipoundwa serikali ya umoja wa kitaifa alikuwa na makaazi yake.
Msemaji
wa kiongozi huyo James Gatdet amesema vikosi vya Rais Silva Kiir
vilishambulia sehemu za Machar huko Jebel.Gatdet ameandika katika
ukurasa wa Facebook kwamba vikosi vyao vimeteka vifaru vitatu kutoka
vikosi vya Kiir vilioshambulia Jebel. Ameongeza kusema kwamba shambulio
lao hilo limezimwa na kwamba mashambulizi yao kwa kutumia helikopta hivi
sasa yamesitishwa baada ya moja ya helikopta hizo nusura iangushwe.
Hali
katika mji huo bado ni tete na kuna mapambano katika baadhi ya maeneo ya
mji huo.Radio Tamazuj ya ndani ya nchi imetangaza kwamba makombora
yaliyofyetuliwa kwa mizinga yameangukia katika kambi ya Umoja wa Mataifa
karibu na Jebel ambapo watu wengi wamejeruhiwa wakiwemo wafanyakazi wa
Umoja wa Mataifa na watu waliopotezewa makaazi yao.
Mfanyakazi
wa misaada aliyezungumza kwa masharti ya kutotajwa jina anakadiria
kwamba watu 10,000 wameukimbia mji huo.Gregor Fischer mpiga picha wa
Ujerumani amesema kulikuwa na mashambuliano makubwa ya risasi wakati wa
asubuhi na kwamba wamekuwa wakisikia milio ya risasi,mizinga na
helikopta zikiruka.Pia ameshuhudia vifaru vya serikali katika mji huo.
Idadi ya vifo ni 270
Maafisa
katika ofisi ya rais wamesema idadi ya vifo imefikia watu 270 tokea
kuzuka kwa mapigano hayo hapo Ijumaa na kwamba kuna majeruhi 210 kwa
upande wa Machar na 60 kwa upande wa Kiir.
Raia
wamekuwa wakikimbilia katika maeneo mawili ya Umoja wa Mataifa na
mashahidi wanasema maelfu ya watu wengine wamekuwa pia wakikimbia kutoka
Juba kuelekea Gurei kama kilomita 20 magharibi mwa mji mkuu.
Hapo
awali ubalozi wa Marekani uliripoti kutokea kwa mapigano katika mji wote
wa Juba ukiwemo uwanja wa ndege.Kutokana na wasi wasi wa hali ya
usalama katika mji huo shirika la ndege la Kenya limetangaza kusitisha
safari zake katika mji mkuu huo.
Pigo kwa amani
Machafuko
hayo yamekuwa yakiendelea tokea Alhamisi wakati mapambano yalipozuka
kati ya vikosi vya serikali na waasi.Hapo Ijumaa mapigano yalizuka
karibu na kasri la rais ambapo Kiir alikuwa akikutana na Machar.
Kuibuka
kwa mapigano hayo kumekuwa pigo kwa matumaini ya amani baada ya makundi
hayo yanayohasimiana kuunda serikali ya umoja wa kitaifa hapo mwezi wa
Aprili wakati nchi hiyo ikiwa ndio kwanza imeadhimisha miaka mitano ya
uhuru wake kutoka Sudan hapo Jumamosi.
Mapambano
ya kuwania madaraka kati ya Kiir na Machar ambayo yaligeuka kuwa
mapamano ya kijeshi hapo mwezi wa Disemba mwaka 2013 yameuwa maelfu ya
watu na kuwapotezea makaazi watu milioni mbili.DW
SHARE
No comments:
Post a Comment