Mabasi ya Shirika la Mabasi yaendayo haraka Dar es Salaam (UDART) yakiwa makao makuu ya Udart Jangwani jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Shirika la Mabasi yaendayo Haraka Dar es Salaam (UDART),
David Mgwassa (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa
habari Dar es Salaam jana, kuhusu matumizi ya kadi badala ya tiketi.
Kulia ni Mkuu wa Idara ya Fedha wa Kampuni ya MaxMalipo walioingia ubia
ma Udart katika mpango huo, Deogratius Lazari.
Mkuu wa
Idara ya Fedha wa Kampuni ya MaxMalipo walioingia ubia ma Udart katika
mpango huo, Deogratius Lazari (kulia), akizungumza katika mkutano huo.
Meneja wa Uhusiano wa Udart, Deus Bugaywa (kushoto), akichangia jambo kwenye mkutano huo.
Mkutano na wanahabari ukiendelea
Na Dotto Mwaibale
SHIRIKA
la Mabasi yaendayo haraka Dar es Salaam (UDART), imetangaza kaunzia
Julai 30 mwaka huu kuwa ni mwisho wa matumizi ya tiketi za kawaida kwa
abiria badala yake zitatumika kadi.
Hayo
yalibainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa UDART, David Mgwassa wakati
akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana asubuhi kuhusu
matumizi ya kadi badala ya tiketi.
" Tiketi
zitaendelea kutumiwa na wanafunzi lakini watu wengine wote watatumia
kadi maalumu za kupandia mabasi yetu" alisema Mgwassa.
Alisema
Udart imepunguza bei ya kadi hizo kutoka sh.4500 ya awali hadi kufikia
sh.2000 ili kutoa fursa kwa kila mwananchi wa kuweza kuipata kadi hizo
na kuzitumia.
Mgwassa alisema kadi ziliuzwa ni 55,000 na zilizobaki ni 150,000.
Mkuu wa
idara ya Fedha wa Kampuni ya MaxMalipo walioingia ubia ma Udart katika
mpango huo, Deogratius Lazari alisema wateja wataweza kulipia kadi hizo
kupitia kwa mawakala wao waliopo katika vituo vyote vya udart na kwa
njia ya mitandao yote ya simu. (P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment