Rais
Magufuli (aliyekaa) akiwa na baadhi ya watendaji wa Ikulu.Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Prof.
Longinus Kyaruzi Rutasitara kuwa Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya
Usafiri wa Anga (TCAA).
Prof.
Longinus Kyaruzi Rutasitara anachukuwa nafasi iliyoachwa wazi na Dkt.
Nyamajeje Calleb Weggoro ambaye muda wake umemalizika.
Uteuzi huu umeanza tarehe 16 Julai, 2016.
Kwa
mujibu wa sheria ya Mamlaka ya usafiri wa anga ya mwaka 1977 Mwenyekiti
na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka hiyo huteuliwa na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo Mwenyekiti akitoka Tanzania Bara,
Makamu Mwenyekiti hutoka Tanzania Zanzibar na kinyume chake.
Wakati
huo huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli amempandisha cheo Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Kedmon
Andrew Mnubi kuwa Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP).
SACP
Kedmon Andrew Mnubi pamoja na makamishna wengine 59 ambao Rais Magufuli
amewapandisha vyeo kuanzia tarehe 16 Julai, 2016 watakula kiapo cha
uadilifu kwa viongozi wa umma kesho jumatatu tarehe 18 Julai, 2016 Ikulu
Jijini Dar es salaam saa tatu asubuhi.
Rais
Magufuli atakuwepo wakati Makamishna wote 60 wakila kiapo cha uadilifu
kwa viongozi wa umma, zoezi ambalo litaendeshwa na Kamishna wa Maadili
Jaji Mstaafu Salome Kaganda.
Wote
watakaohudhuria tukio hili wanatakiwa kufika Ikulu kabla ya saa mbili na
nusu asubuhi na wataingia kupitia lango kuu la mashariki (lango la
baharini).
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
17 Julai, 2016 (P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment