Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akihutubia wakati wa Uzinduzi wa Ripoti ya Lishe ya Dunia kwenye mkutano
uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu
akizungumza kwenye mkutano wa kuzindua ripoti ya lishe ya Dunia ambao
mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Samia
Suluhu Hassan.
Baadhi ya Wadau wakifuatilia kwa makini mkutano huo wa uzinduzi ya ripoti ya Lishe ya Dunia.
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
(kulia) akikata utepe kuashiria kuzindua ripoti ya Lishe ya Dunia,
katkati ni Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto
Mhe.Ummy Mwalimu na Mkurugenzi Mtendaji wa PANITA ,Dkt. Tumaini Mikindo
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema
serikali ya awamu ya TANO itatoa msukumo mkubwa katika kukabiliana na
tatizo la utapiamlo nchini kwa kuweka mipango na mikakati imara ikiwemo
kuongeza bajeti ya lishe, kuongeza virutubisho kwenye vyakula na kutumia
vyema wataalamu wa lishe katika kupambana na tatizo hilo hapa nchini.
Makamu
wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam Trh
20-Jul-16 katika hotuba yake ya uzinduzi wa Ripoti ya Dunia ya
Utapiamlo ambayo imetilia mkazo masuala ya lishe kama msingi wa Maendeleo hapa nchini na Duniani kwa ujumla.
Makamu
wa Rais amesema viongozi wa serikali katika ngazi zote za wilaya na
mikoa wanatakiwa kuunga mkono jitihada za kuondoa utapimlo nchini kwa
kuweka msukuko wa kipekee katika ngazi zote za maamuzi.
Ameeleza
kuwa jitihada zinazofanywa na serikali kwa ushirikiano na wadau wa
Maendeleo wa Ndani na Nje ya Nchi zimesaidia kwa kiasi kikubwa kushusha
kiwango cha udumavu nchini kutoka asilimia 42 mwaka 2010 hadi kufikia
asilimia 34 mwaka 2015.
Amefafanua
kuwa kutokana na mafanikio hayo, serikali imetoa mwongozo wa bajeti ya
mwaka 2016/17 kwa kutenga kiasi cha shilingi milioni 500 kwa ajili ya
masuala ya lishe kwa kila mtoto wa umri chini ya miaka MITANO hapa
nchini Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema pamoja na fedha hiyo
kuwa kidogo lakini serikali itaendelea kuongeza kiasi cha fedha kwenye
bajeti zijazo hadi kufikia kiasi cha dola 8.5 sawa na shilingi elfu
18000 kwa kila mtoto hapa nchini kama ilivyoshauriwa na jopo la wataalamu wa Benki ya Dunia na wa masuala ya afya na uchumi duniani.
Makamu wa Rais pia ameziagiza Halmashauri zote Nchini kupitia TAMISEMI zihakikishe zinatumia fedha hizo vizuri na kwa malengo yaliyokusudiwa na sio vinginevyo. (P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment