Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir na Makamu wake wa kwanza Riek Machar, katika Ikulu ya Juba, Aprili 26, 2016
Waziri wa
Habari na msemaji wa serikali ya Sudan Kusini Michael Makuei Lueth
amesema nafasi ya Makamu wa kwanza ya rais Riek Machar ambaye aliondoka
jijini Juba baada ya kuzuka kwa mapigano wiki mbili zilizopita, inaweza
kuchukuliwa na mtu mwingine kutoka upande wake kwa mujibu wa mkataba wa
amani uliotiwa saini mwaka uliopita.
Kumekuwa
na uvumi jijini Juba kuwa huenda nafasi ya Machar ikachukuliwa na
mwanasiasa mwingine ikiwa hatarejea Juba kwa mujibu wa Gazeti la Sudan
Trubune.
Wakati
huo huo, rais Salva Kiir amesema nchi yake haitakubali kuongozwa kwa
wanajeshi wa kulinda amani nchini humo baada ya Umoja wa Afrika
kupitisha azimio la kutumwa kwa wanajeshi wa kulinda amani nchini Sudan
Kusini.
Hali ya
wasiwasi imeendelea kuripotiwa nchini Sudan Kusini baada ya kutokea kwa
mapigano makali kati ya wanajeshi wa serikali na wale wanaomuunga mkono
Makamu wa rais Riek Machar. Licha ya pande mbli, Salva Kiir na Riek
Machar, kuwasihi wanajeshi wao kusitisha mapigano na kurejea makambini,
raia bado wana hofu ya kutokea kwa mapigano mengine.(P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment