
Mkutano
wa kilele wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO umeanza mjini Warsaw, huku Rais
Barack Obama akiwataka viongozi hao kusimama imara dhidi ya kuibuka
upya kwa Urusi na kutotikiswa na Uingereza kujiengua Umoja wa Ulaya.
Katika
makala yake kwenye jarida la Financial Times iliyochapishwa leo, muda
mchache kabla ya kuanza mkutano huo wa kilele, Obama amewataka viongozi
wa Ulaya kusimama thabiti dhidi ya hatua ya Urusi ya kuutwaa mkoa wa
Crimea uliokuwa sehemu ya kundi la kigaidi linalojiita Dola la Kiislamu,
IS, na changamoto nyingine zinaikabili jumuiya hiyo ya kiusalama, hasa
katika kipindi hiki ambacho Uingereza inatishia kuondoka katika Umoja wa
Ulaya.
Hata
hivyo, ikulu ya Urusi, Kremlin, imetoa taarifa yake ikisema kuwa
inatazamia akili ya kawaida itatawala kwenye mkutano huo wa kilele wa
NATO, na ikitupilia mbali hoja ya NATO kuichukulia Urusi kuwa ni kitisho
kwao.
Msemaji
wa Kremlin, Dmitry Peskov, amesema Urusi imekuwa na itaendelea kuwa
tayari kwa majadiliano na NATO wakati wowote na pia kushirikiana nayo.
Rais
Obama aliyewasili katika mkutano wake huo wa mwisho wa NATO kabla ya
kuachia madaraka, amesema anaamini kwamba kujitoa kwa Uingereza,
kutaifanya Jumuiya hiyo ya kujihami kuwa kiungo muhimu zaidi cha
kuwaunganisha wanachama waliosalia wa umoja wa Ulaya.

Rais Barack Obama alipofungua mkutano huo
"Ninaamini
kwamba mataifa yetu yatatakiwa kukusanya nguvu ya kisiasa na kuwa na
msimamo thabiti katika kukabiliana na changamoto zilizopo. Naamini
tunaweza, lakini tu iwapo tutasimama pamoja kama washirika wamoja" Obama
aliandika.
Matamshi
ya Obama yametolewa ijumaa hii baada ya kufungua mkutano wa siku mbili
unaowakutanisha viongozi wa Umoja wa Ulaya na wa jumuiya ya kujihami ya
NATO, unaofanyika mjini Warsaw, Poland. Obama alifanya ufunguzi huo
pamoja na rais wa Baraza la Umoja wa Ulaya, Donald Tusk na rais wa
kamisheni ya umoja huo, Jean-Claude Junker.
Mataifa
28 ya Jumuiya hiyo Ijumaa hii watakubaliana rasmi kupeleka vikosi vinne
vya wanajeshi vitakavyokuwa na askari kati ya 3000 hadi 4000 katika
mataifa ya Baltiki na Poland ya Magharibi, ikiwa ni sehemu ya mpango
wake wa kawaida wa kuhakikisha utayari wake wa kuwalinda wanachama wake
wa Magharibi.
Licha ya
Rais Vladimir Putin wa Urusi kuonekana kupuuzia hali ya wasiwasi
iliyotawala mkutano huo, atahudhuria mkutano kati ya Urusi na NATO wiki
ijayo, huo ukiwa ni mkutano wa pili ulioshinikiza Urusi kuiachia Crimea
mnamo mwaka 2014. Urusi iliyaruhusu makubaliano yaliyofikiwa na Umoja wa
Mataifa yaliyotoa mamlaka kwa Umoja wa Ulaya kuingilia biashara ya
silaha zilizopelekwa Libya kupitia bahari ya Mediterania.
Katibu
Mkuu huyo ameelezea imani yake kwamba kujiondoa kwa Uingereza ya kwenye
Umoja wa Ulaya, hakutaathiri mahusiano na Marekani, na kusema kuwa
Uingereza bado itaenedelea kuwa mwanachama hai kwenye Jumuiya hiyo ya
kiusalama.DW
SHARE
No comments:
Post a Comment