
Sweetbert Lukonge,GPL
Dar es Salaam
OFISA
Habari wa Simba, Haji Manara, hivi karibuni alipata matatizo ya macho
baada ya jicho lake moja kupoteza uwezo wa kuona, wakati akiendelea na
matibabu, wanachama wa Yanga wameamua kumchangia fedha za matibabu
katika kile walichodai kuonyesha michezo siyo uadui.
Wanachama
hao wameongozwa na Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Yanga,
Jerry Muro ambaye alithibitisha juu ya mchango huo kwa kusema kuwa
wamefikia uamuzi huo kutokana na kuguswa zaidi na tatizo hilo ambalo
limempata Manara kama ndugu na mdau mkubwa katika soka nchini.
“Soka
siyo uadui bali ni mchezo unaotuweka pamoja, pia upinzani wa Simba na
Yanga upo uwanjani ila nje ya uwanja sisi sote ni ndugu, tatizo
alilopata Manara ni kubwa.
“Kutokana
na hali hiyo tukiwa kama wanafamilia wenzake na ndugu zake imetubidi
tuchangishane ili kuhakikisha tunapata kiasi fulani cha fedha
kitakachomsaidia katika matibabu yake.
“Tumepanga
kuwa kama ataenda nje ya nchi basi gharama zote za nauli ya kwenda na
kurudi ziwe kutoka kwa wanachama na mashabiki wa Yanga, hata hivyo mpaka
sasa tumeshachangishana zaidi ya shilingi milioni moja na bado
tunaendelea,” alisema Muro na kuongeza:
“Fedha hizo tutamkabidhi siku yoyote ile kuanzia leo mara tu tutaka-pokutana kwa pamoja na waratibu wa zoezi hili.”
Alipotafutwa
Manara ili aweze kuzungumzia suala hilo hakuweza kupatikana kufuatia
simu yake ya mkononi kuita tu bila ya kupokelewa.(P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment