Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete-JKCI- Profesa William Mahalu( katikati) akiwasili ndani taasisi hiyo kwa mara ya kwanza tangu ateuliwe na Rais John Magufuli , kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI , Profesa Mohamed Janabi na kulia ni Afisa Uhusiano wa Taasisi hiyo Maulid Kikondo.
Profesa William Mahalu akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete Profesa Mohamed Janabi akielezea utendaji kazi wa taasisi hiyo .
Baadhi ya viongozi wa Taasisi ya JKCI wakimsikiliza Profesa Mahalu wakati akizungumza nao mara baada ya kujitambulisha .
……………………………………………………………………………………………….
Dar es salaam,
Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Moyo ya Jakay Kikwete JKCI- Profesa William Mahalu kwa mara ya kwanza tangu ateuliwe na Rais John Magufuli kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya taasisi hiyo ametembelea JKCI kwa lengo la kujitambulisha na kuzungumza na viongozi.
Katika mazungumzo hayo amewataka viongozi wa taasisi hiyo kuwa mfano na kufanya kazi kwa bidii ili kuendana na kasi ya Rais John Magufuli ya hapa kazi tu.
Pia amewapongeza kwa kazi kubwa wanayoifanya katika kuhakikisha watanzania wenye magonjwa ya Moyo wanapatiwa matibabu hapa hapa nchini hatua ambayo imepunguza gharama kubwa ya kugharamia matibabu nje ya nchi.
SHARE









No comments:
Post a Comment