Kamishina wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, Simon Sirro akiongea na wanahabari (hawapo pichani).
Akionesha bunduki iliyokamatwa.
Kamanda Sirro akionesha vyeti bandia vya sekondari.
Nyaraka na vyeti mbalimbali vilivyokamatwa na jeshi la polisi jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya vyeti Bandia vya Mamlaka ya Mapato (TRA) vilivyokamatwa.
JESHI la
polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limekamata mitambo na vyeti
mbalimbali vya shule za msingi, kuzaliwa, sekondari, biashara, stika za
magari za TRA, bunduki moja na bastola maeneo mbalimbali ya jiji la Dar
es salaam ikiwemo eneo la Pugu.
Akizungumza
na wandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,
Kamishna Simon Sirro amesema kuwa vyeti hivyo na mitambo ya kuchapisha
ilikamatwa katika oparesheni maalum iliyofanyika Julai mwaka huu, huku
taarifa zingine zikitolewa na wananchi kukabiliana na waharifu hao.
Amesema
majambazi waliokamatwa bado majina yao yanahifadhiwa kwa ajili ya
uchunguzi zaidi na watuhumiwa wa vyeti bandia bado wanaendelea kuhojiwa
na uchunguzi ukikamilika watafikishwa mahakamani.
Kamishna
Sirro amewataka wale wote wanaotumia vyeti bandia kujisalimisha kabla ya
oparesheni kali itakayowachukulia hatua kuanza kwani inaonesha
watuhumiwa baada ya kubanwa waliwataja baadhi ya vigogo waliotengenezewa
vyeti hivyo na kuajiriwa serikalini na taasisi zingine.(P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment