Wanajeshi na askari polisi wakipiga doria katika mtaa mmoja wa Bujumbura, Februari 3, 2016.
Mazungumzo
juu ya mustakabali wa Burundi yaliyokua yatanatazamiwa kuanza Jumanne
hii Julai 12 katika mji wa Arusha, nchini Tanzania yamegubikwa na hali
ya sintofahamu, baada ya wajumbe wa Serikali na wale wa chama tawala
CNDD-FDD kususia uzinduzi wa mazungumzo hayo mapema mchana.
Mazungumzo
hayo yanafanyika ili kujaribu kuindoa nchi hiyo katika mgogoro
unaoendelea. Kwa kikao hiki cha pili, Rais wa zamani wa Tanzania
Benjamin Mkapa anaukutanisha utawala wa Bujumbura, upinzani uliolibaki
Burundi, na baadhi ya wanaharakati wa vyama vya kiraia.
Hali hiyo
imeibuka baada ya baadhi ya wanasiasa kutoka kambi ya upinzani walio
uhamishoni na wanaharakati wa vyama vya kiraia walioanzisha maandamano
dhidi ya muhulawa tatu wa Rais Pierre Nkurunziza kupewa mwaliko wa
kushiriki mazungumzo hayo. Watu hao ni pamoja na Jean Minani, kiongozi
wa muungano wa wanasiasa wa upinzani walio uhamishoni (CNARED) na
wanaharakati watatu, ambao ni miongoni mwa waanzilishi wa maandamano
dhidi ya muhula watatu wa Rais Pierre Nkurunziza, ikiwa ni pamoja na
Armel Niyongere na Pacifique Nininahazwe.
Wajumbe
wa Serikali ya Bujumbura wanasema kuwa watu hao walishiriki katika
jaribio la mapinduzi yaliyotibuliwa Mei 13 na 14 mwaka 2015.
Mshauri
mkuu wa Rais Nkurunziza katika masuala ya mawasiliano, Willy Nyamitwe,
amesema Jean Minani, Armel Niyongere na Pacifique Nininahazwe
wanatafutwa na vyombo vya sheria vya Burundi, kwa hiyo hawawezi kualikwa
katika mazungumzo ya Arusha.
CNARED bado haijatambuliwa ...
Serikali
ya Burundi imeendelea kusema kuwa mashauriano tayari yameanza nchini
Burundi baina ya Warundi. Tume iliyoteuliwa na utawala wa Bujumbura kwa
minajili ya kuendesha maungumzo baina ya wadau walio ndani ya nchinii
inaendelea na mazungumzo tangu miezi kadhaa, na kuweza kufikia katika
uundwaji wa Katiba mpya.
Serikali
inasema, wale utawala wa Bujumbura unawachukulia kama "magaidi"
wametengwa katika mashauriano hayo. Serikali, hapo, inalenga muungano wa
wanasiasa wa upinzani (CNARED). Hakuna mazungumzo yanayowezekana:
serikali ya Bujumbura inakataa katu katu kukaa kwenye meza moja na
CNARED.
Mwishoni
mwa juma hili, msuluhishi katika mgogoro wa Burundi, Benjamin Mkapa
atawasilisha mpangilio wa mazungumzo kwa Marais wa nchi za Jumuiya ya
Afrika Mashariki, nje ya mkutano wa Umoja wa Afrika mjini Kigali.RFI
SHARE
No comments:
Post a Comment