Mwakilishi
Maalumu wa masuala ya maji kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa Elimu,
Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Watu wa
Kenya Mwai Kibaki (kushoto) akisalimiana na Mwenyekiti wa Kamati ya
maandalizi ya Maonesho ya Wiki ya Maji Afrika (Sylivester Matemu) wakati
wa maonesho ya sita katika ya wiki ya maji Afrika yanayoendelea jijini
Dar es salaam. Katikati ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na
Umwagiliaji Mhandisi Emmanuel Kalobelo.
Mwakilishi
Maalumu wa masuala ya maji kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa Elimu,
Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Watu wa
Kenya Mwai Kibaki akisalimia na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na
Umwagiliaji Mhandisi Emmanuel Kalobelo leo jiji Da es salaam.
Katibu
wa Mwakilishi Maalumu wa masuala ya maji kutoka Shirika la Umoja wa
Mataifa Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na Rais Mstaafu wa Jamhuri
ya Watu wa Kenya Mwai Kibaki (katikati), Profesa Nick Wanjohi akifafanua
jambo kwa mwakilishi huyo alipotembelea na daraja la Mwalimu Nyerere
linalounganisha eneo la Kigamboni kupitia bahari ya Hindi na eneo la
katikati ya jiji la Dar es salaam.
Mwakilishi
Maalumu wa masuala ya maji kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa Elimu,
Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Watu wa
Kenya Mwai Kibaki (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya
viongozi walioandamana kutembelea daraja la Mwalimu Nyerere
linalounganisha eneo la Kigamboni kupitia bahari ya Hindi na eneo la
katikati ya jiji la Dar es salaam. (Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO)
Mwakilishi
Maalumu wa masuala ya maji kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa Elimu,
Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Watu wa
Kenya Mwai Kibaki ametembelea mabanda ya maonesho ya sita katika ya wiki
ya maji Afrika yanayoendelea jijini Dar es salaam.
Katika
tukio hilo Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Mhandisi
Emmanuel Kalobelo amimweleza Mwakilishi huyo kuwa Tanzania imejipanga
kuhakikisha kuwa hadi ifikapo 2020 iweze kufikisha maji kwa wananchi
wote kwa maendeleo yao na taifa kwa ujumla.
Mhandisi
Kalobelo aliongeza kuwa hatua hiyo itaifanya Tanzania kufikisha maji kwa
wakazi wa mijini kwa asilimia 95 na kwa wakazi wa vijijini kw asilimia
85.
Aidha,
katika hatua nyingine, Mwakilishi huyo alitembelea barabara iliyopewa
jina la Mwai Kibaki inayoanzia eneo la Morocco hadi njia panda ya Kawe
jijini Dar es salaam pia alitembelea na daraja la Mwalimu Nyerere
linalounganisha eneo la Kigamboni kupitia bahari ya Hindi na eneo la
katikati ya jiji la Dar es salaam.
Maonesho
ya sita katika ya wiki ya maji Afrika mwaka huu yanayoendelea jijini Dar
es salaam yanaongozwa na kaulimbiu inayosema “Kufikia lengo la Mendeleo
Endelevu (SDGs) juu ya Usalama wa Maji na Usafi wa Mazingira”.(P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment