Na Masanja Mabula –Pemba ..
KOCHA
Mkuu wa Klabu ya Kizimbani United Bakar Ali Kilambo , amewashauri
viongozi wa vilabu Kisiwani Pemba kuwalipia gharama za masomo makocha
ambao wameonyesha nia ya kujiendeleza ili baadaye watumnike katika
kuzifundisha vilabu husika .
Akizungumza
na mwandishi wa habari hizi Kilambo alisema , baadhi ya viongozi wa
timu wanatumia fedha nyingi kuwalipa waganga badala ya walimu (kocha)
jambo linapelekea baadhi ya timu kufundishwa na walimu wasio na sifa
inayotakiwa na ZFA.
Alisema
kwamba ingekuwa ni jambo la busara kwa uongozi wa klabu kuwalipia
gharama za masomo baadhi ya nyota wake walioonesha nia ya kujiendeleza
kwa kusoma kozi ya ukocha , ili baadaye waweze kutoa msaada wao wa
kiufundi na kuondoa changamoto ya vilabu kufundishwa na walimu walio na
sifa .
Alisema ,
vijana wengi wanaotaka kusoma kozi ya uwalimu wa mpira wa miguu
wanakabiliwa na changamoto ya ukosrfu wa fedha za kulipia kozi hizo ,
ambazo zimekuwa zikiandaliwa na ZFA kwa kushirikiana na chama cha
makocha .
“Viongozi
wa vilabu vyetu vinathamini sana waganga na wanatumia fedha nyingi
kuwalipa , mimi ningewashauri viongozi kuwalipia gharama za masomo ya
ukocha vijana ambao wanataka kujiendeleza kusoma kozi ya ukocha ”
alishauri.
Katika
hatua nyingine kocha Kilambo amewataka vijana wanaotaka kujiendeleza kwa
kusoma kozi ya ukocha kuchangamkia fursa zinazotolewa na ZFA kwa
kushirikiana na TFF ambazo zimelenga kuinua taaluma hiyo hapa nchini .
Alisema
pamoja na hali ya umaskini inayowakabili , lakini wanatakiwa kuagalia
umuhimu wa taaluma hiyo katika kuwajenga vijana kuweza kujipatia ajira
kupitia medani ya michezo .
“Hivi
karibu kumeandalia kozi ya ukocha , ni vyema vijana wanaohitaji taaluma
hii kuitumia fursa hii kuhakikisha wanajiunga ili wapate ujuzi ambao
baadaye watautumia kama ajira ya kujiupatia kipato”alieleza.
Uchunguzi
uliofanywa na mwandishi wa habari hizi umebaini kwamba vijana wengi
wanaotaka kujiendeleza kwa kusoma kozi ya ukocha wanashindwa kufanya
hivyo kutokana na kozi hizo kuwa na gharama kubwa huku kipato chao ni
kidogo .(P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment