Naibu
Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh,Luhaga Mpina
akisikiliza kero za wanainchi wa boko zinazosababishwa na kiwanda cha
Twiga cement kilichopo wilaya ya kinondoni jijini Dar es salaam.
Naibu
Wazirgi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh Luhaga Mpina
akiwa katika ziara ya ukaguzi wa mazingira katika kiwanda Royal soap
kilichopo mabibo jijini dare s salam.
Hili ni
eneo la kiwanda linalotiririsha maji kutoka kiwanda cha kutengeneza
sabuni kilikchopo mabibo jijini Dar es salaam kinachotuhumiwa
kutiririsha maji machafu katika mto kibangu uliopo ubungo kibangu.
Serikali kupitia Baraza laTataifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC imekitoza faini ya
shilingi milioni kumi, kiwanda cha kutengeneza sabuni cha Royal Soap industry cha Mabibo jijini
Dar es Saal kwa kosa la kutiririsha maji machafu na yenye sumu sambamba na vumbi la sabuni lenye kusambaa katika makazi wa watu na mazingira ya mto kibangu.
Uchafuzi huo wa mazingira umekuwa ni wa muda mrefu katika makazi ya mtaa wa mabibo kisimani na kupelekea afya za wakazi wa eneo hilo kuwa hatarini, kutokana na maji machafu yenye kemikali na vumbi la sabuni, na kupelekea wananchi wa mtaa huo wa kibangu kupeleka malalamiko yao katika Ofisi ya Makamu wa Rais, na ndipo Naibu Waziri wa Ofisi Hiyo anaeshunghuliakia masuala ya Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Joelson Mpina, kuinuka ofisini na kwenda kujionea adha wanayoipata wakazi hao.
Naibu Waziri Mpina alilielekeza Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC kufuatilia vipimo vya vumbi na maji ya sabuni yanayotiririka katika mazingira na mto kibangu, kama ni rafiki kwa mazingira na viumbe hai na kuwasilisha taarifa hiyo ndani ya siku kumi na nne sanjari na kukitoza faini ya shilingi milioni kumi kiwanda hicho na kukitaka kilipe kwa muda huo wa wiki mbili, kwa kosa la kukiuka sheria ya mazingira na kanuni zaake ya mwaka 2004.
Naibu Waziri Mpina, yupo kwenye ziara ya ukaguzi wa mazingira na kufuatiliaji na uzingatiaji wa sheria
SHARE
No comments:
Post a Comment