Naibu balozi wa Ubalozi wa China Bw. Gou Haodong akizungumza katika uzinduzi wa duka la simu jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Faustin Kamuzora akiwa katika picha ya pamoja.
Katibu Mkuu
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Faustin Kamuzora
akikata utepe kuashiria uzinduzi wa duka jijini Dar es Salaam.
KATIBU
Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Faustin Kamuzora
ameipongeza kampuni ya Huawei Tanzania katika juhudi zake endelevu za
kuleta teknologia ya mawasiliano yenye kiwango cha juu kwa watanzania,
kufuatia uzinduzi rasmi wa duka la 7 la bidhaa za Huawei na kitengo cha
huduma kwa wateja katika duka la Mlimani City, Dar es Salaam mwishoni
mwa wiki iliyopita.
Mapema
mwaka huu Huawei Tanzania walianzisha mpango wao wa kuongeza mtandao
wao wa usambazaji nchini kote kwa kuongeza maduka ya bidhaa zao nchini
kote. Uzinduzi wa duka la bidhaa zake la Mlimani City ni mwitikio wa
uhitaji unao ongezeka wa bidhaa za Huawei nchini na kuhakikisha kuwa
bidhaa za Huawei na huduma zake zinapatikana kwa urahisi kwa wateja wa
Tanzania.
Tangu
mwanzoni mwa mwaka huu Huawei Tanzania imefanikiwa kuzindua maduka 7 ya
bidhaa zake na kuongeza idadi ya mawakala wake nchini. Miongoni mwa
maduka hayo ni duka liliolopo Mtaa wa Samora, City Mall na JM Mall
jijini Dar es Salaam na maduka mengine mengi katika mikoa ya Mwanza,
Arusha na Mbeya.
Huawei
Tanzania inatarajia matokeo mazuri katika duka lake la Mlimani City na
kitengo cha huduma za simu kufuatia mauzo mazuri na huduma
vilivyodhihirishwa na maduka mengine ya Huawei nchini kote. Duka hili la
7 la bidhaa za Huawei na kitengo cha huduma kwa wateja la Mlimani City
ndilo kinara cha maduka yote ya Huawei Tanzania. Duka hili linawaahidi
watanzania bidhaa na huduma za ubora wa juu kabisa.
Huawei
imekuwa mstari wa mbele daima katika ubunifu na mabadiliko ya
kiteknolojia kwa kwenda sambamba na mabadiliko na mahitaji ya wateja.
“Tumehakikisha
kuwa tunakidhi kila mahitaji ya wateja wetu, hata hivyo tumeenda mbali
zaidi kwa kuzingatia tofauti za vipato vyao na matumizi kwa kuwaletea
bidhaa ambazo zitakidhi haja ya kila mteja wetu”. Alidhihirisha
Mkurugenzi Mtendaji wa Huawei Tanzania Bw. Levin Zhang (Yongquan),
katika hotuba yake ya sherehe ya ufunguzi.
“Huawei
Tanzania imewekeza kwa kiasi kikubwa nchini na imejikita katika
kuhakikisha ukuaji na maendeleo ya sekta ya mawasiliano nchini. Tangu
kuanzishwa kwa shughuri zetu nchini, tumeshirikiana na sekta mbalimbali
ikiwamo serikali katika kuipeleka mbele TEHAMA. Huawei Tanzania
imedhamiria kuwa kinara wa simu za kisasa Tanzania, kwa kuwapatia wateja
wake simu bora na zinazotumika kwa urahisi.” Alidhihirisha mkurugenzi
huyo.
Akiwahutubia
wananchi wakati wa uzinduzi huo, Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano Prof. Faustin Kamuzora ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi
aliipongeza kampuni ya Huawei Tanzania kwa hatua waliyoichukua ya kuinua
sekta ya TEHAMA nchini. Katibu mkuu huyo amepongeza juhudi zilizofanywa
na Huawei Tanzania si tu katika kuleta mawasiliano bora na teknolojia
kwa kupitia bidhaa zao nyingi za simu za kisasa bali pia kwa kuwezesha
upatikanaji wa fursa za ajira kwa watanzania.
“Kwa
miaka mingi sasa serikali ya Tanzania imekuwa na uhusiano mkubwa na
Huawei Tanzania, na tumeshirikiana na kampuni hii katika miradi mingi
kwa mafanikio makubwa. Kwa kupitia ubunifu wao katika eneo la TEHAMA,
Huawei imeendelea kuwa na mchango mkubwa kwa nchi yetu. Ufunguzi wa duka
hili hapa Mlimani City ni hatua ya mwendelezo wa juhudi zake kwa wateja
wake wa Tanzania ambao wanauhitaji mkubwa wa teknolojia ya
mawasiliano.
Nina
matumaini kuwa kwa kupitia hatua mabalimbali ambazo serikali imechukua
katika kukabiliana na changamoto zinazoikabili TEHAMA na kwa mwendelezo
wa ushirikiano wa wadau binafsi kama Huawei Tanzania, malengo yetu ya
Milenia ya kuwawezesha watanzania kwa kupitia TEHAMA yatafikiwa”.
Alisema Katibu Huyo.
Naibu
balozi wa Ubalozi wa China Bw. Gou Haodong ambaye alishiriki sherehe za
uzinduzi ameipongeza Huawei Tanzania kwa hatua yake muhimu ya kuboresha
sekta ya mawasiliano ya simu nchini.
“Nina
matumaini kuwa kampuni hii kubwa kutoka China itaendelea kuwekeza katika
sekta ya mwasiliano hapa Tanzania. Naamini, kwa juhudi za pamoja baina
ya serikali na Huawei zitaifanikisha Tanzania kuifikisha sekta hii
katika viwango vya juu”. Alisema
Serikali
ya Tanzania inatambua mchango wa Huawei katika kuhakikisha upatikanaji
wa simu halisi hapa nchini. Kampuni hii pia imeendesha miradi kadha wa
kadha ya kuendeleza vipaji vya TEHAMA nchini ambayo imewajengea uzoefu
wnafunzi wa kitanzania na kuwaandaa kufanya kazi katika makampuni ya
simu. Huawei pia imeteuliwa kuwa mshauri wa serikali wa TEHAMA, mradi
ambao utaipa nafasi Huawei ya kutoa mafunzo ya TEHAMA, elimu na huduma
kubwa za data.
Katika
kusherehekea uzinduzi huu wa duka la bidhaa za Huawei Mlimani City,
Huawei Tanzania inatoa punguzo maalum kwa aina kadhaa za simu kuanzia
Julai 16 hadi 31. Huawei pia imetangaza uwepo wa tolea lake jipya kabisa
lenye teknolojia ya juu zaidi la Huawei P9 katika soko la Tanzania. P9
ni simu ya kwanza duniani yenye kamera mbili, inayounda picha zenye
kiwango cha juu kabisa. Kila bidhaa ya Huawei imekuwa ikibadili ubora
katika ulimwengu wa simu katika hadhi na utendaji wake. Huawei P9
imeundwa kwa ajili ya kuleta mapinduzi ya upigaji wa picha kwa simu
katika viwango vipya.
SHARE
No comments:
Post a Comment