Mkurugenzi
Mkuu wa CEORT ( Ceo Roundtable of Tanzania) Santina Benson (kushoto)
na Mshauri Mkuu wa maswala ya sera wa kampuni ya The Nature Conservancy
,Lucy Magembe,(Kulia) wakimsikiliza kwa makini Meneja wa kuboreshaji
Utendaji Kazi Kiwandani wa TBL, , Charles Nkondola (katikati) wakati
alipokuwa akitoa akichangia mada kwenye mkutano wa kimataifa wa maji.
Maneja wa
kuboreshaji Utendaji Kazi Kiwandani wa Uzalishaji wa TBL Group ,
Charles Nkondola (wa pili kulia) akifafanua jambo kwa wadau wa maji
wakati alipokuwa akitoa mada kwenye mkutano wa kimataifa wa maji.
Baadhi ya
washiriki wa mkutano uliowahusisha wadau wa sekta binafsi kushiriki
katika mjadala wa wadau juu ya usimamizi wa rasmali za maji
ulioandaliwa na 2030 Water Resources Group (WRG) na Wizara ya Maji na
Umwagiliaji wakifuatilia mada kwenye ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha
Kimataifa cha Julius Nyerere mjini Dar es Salaam.
Na Mwandishi Wetu
-yawasilisha
mikakati yake ya utunzaji maji kupitia moja ya lengo inalotekeleza
katika uzalishaji lijulikanalo kama “kujenga dunia imara na dunia iliyo
safi’
Kampuni
ya kutengeneza vinywaji ya TBL Group iliyopo chini ya kampuni mama ya
kimataifa ya SABMiller imefanikiwa kutekeleza mpango wa uzalishaji
unaozingatia utunzaji wa mazingira,matumizi mazuri ya maji na kunufaisha
jamii zilizopo maeneo ilipowekeza kwa kujenga viwanda vyake.
Hayo
yamebainishwa na Meneja wa Kuboresha Utendaji kazi Viwandani wa kampuni
hiyo,Bw. Charles Nkondola wakati akichangia mada kuhusiana na matumizi
sahihi ya maji kwenye mkutano wa pembeni wa wataalamu wa sekta ya maji
katika ukumbi wa wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius
Nyerere mjini Dar es Salaam.
Wataalamu
hao kutoka nchi mbalimbali wanahudhuria mkutano mkutano wa Kimataifa
wa maadhimisho ya sita ya Wiki ya Maji Barani Afrika unaoendelea jijini
Dar es Salaam ukiwa unajumuisha wadau mbalimbali katika sekta ya maji.
Alisema
mpango wa uzalishaji wenye tija wa kampuni ya SABMiller ujulikanao kama
Manufacturing Way ambao unatekelezwa na viwanda vyake vyote kwa muda
mfupi umeonyesha kuwa na mafanikio ambapo taasisi nyingi zinatembelea
viwanda vyake kwa ajili ya kujifunza.
Bw.Nkondola
alisema kuwa viwanda vya kampuni ya TBL Group uendeshaji wake unafuata
mifumo bora na kuhakikisha jambo lolote linalofanyika linaenda
sambamba na malengo yaliyowekwa na kampuni mama ya SABMiller ambayo
mtazamo wake unaelekeza kwenye utunzaji wa mazingira ,kutunza vyanzo
vya maji na matumizi mazuri ya maji na kufanya uzalishaji usio na athari
kwa mazingira vilevile kuhakikisha jamii zilizopo maeneo ya kiwanda
zinanufaika na uwekezaji.
Katika
kuhakikisha suala la maji linapewa kipaumbele Bw.Nkondola, alisema
kampuni inatekeleza lengo linalojulikana kama ‘kujenga dunia imara na
dunia iliyo safi’ ambalo limelenga kupata raslimali ya maji ya kutosha
ambao yanatumika kwa kiasi kikubwa katika biashara ya kampuni.
“Katika
kutekeleza lengo hili kampuni kwa muda mrefu imekuwa mstari wa mbele
kulinda na kutunza vyanzo vya maji na kuhakikisha maji yanayopatikana
yananufaisha jamii ya wananchi inayowazunguka ikiwemo kusaidia
kuendeleza miradi ya maji.
Malengo
mengine ya SABMiller ni ‘dunia yenye nuru njema,lengo hili limelenga
kuharakisha ukuaji wa kampuni na maendeleo ya kijamii katika mfululizo
wake wa maadili. ‘kujenga dunia changamfu’ ambalo linalenga kuifanya bia
kuwa kinywaji cha asili kwa mnywaji na kuondoa dhana kuwa unywaji wa
bia ni ulevi, bali kuhamasisha unywaji ambao utawezesha kuwepo wanywaji
wa wastani kwenye jamii ambao pia watazingatia kutekeleza majukumu
yao.
Lengo lingine ni kujenga dunia yenye nguvu kazi lengo kubwa likiwa ni kusaidia matumizi bora na endelevu ya ardhi .
Bw.Nkondola
alisema malengo haya ambayo baadhi yake yanashabihiana na malengo
endelevu ya Umoja wa Mataifa yanadhihirisha kuwa kampuni ya TBL Group ni
kampuni ambayo inalipa kipaumbele suala la utunzaji mazingira,kutunza
vyanzo vya maji na matumizi sahihi ya maji na alisema itaendelea kuunga
mkono jitihada zinazofanywa na serikali na wadau wengine wa sekta ya
maji kuhakikisha maji yanaendelea kupatikana na matumizi mazuri ya
raslimali hii.(P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment