Donald Trump
Donald
Trump ateuliwa kuwa mgombea urais kwa tiketi ya chama cha Republican,
uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwezi November mwaka huu. Trump amepata
uungwaji mkono na wajumbe kutoka majimbo na wilaya za Marekani katika
kura mchujo wa kumpata mgombea wa nafasi hiyo kupitia chama chake cha
Republican kupitia mkutano mkuu wa chama chake mjini Cleveland.
Baada ya
kuchaguliwa kuwa mgombea urais Donald Trump alitoa shukran zake kupitia
mtandao wa twitter,na imetanabahishwa kwamba gavana wa jimbo la Indiana
Mike Pence, ndiye mgombea mwenza .Taarifa zaidi zinasema watoto wawili
wa Donald Trump wa kiume Donald na pia bintiye Tiffany wanatarajiwa
kuhutubia mkutano mkuu wa wanachama wa chama hicho .BBC
SHARE
No comments:
Post a Comment