Naibu
Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrul
(wa nne kushoto), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana,
wakati akitoa msimamo wa chama hicho kuhusu mikakati ya Jeshi la Polisi
dhidi ya vyama vya siasa hasa cha Cuf. Wengine ni maofisa mbalimbali wa
chama hicho.
Naibu
Katibu Mkuu wa chama hicho, Tanzania Bara, Shaweji Mketo, akizungumza na
waandishi wa habari Dar es Salaam , wakati wa kutoa msimamo wa chama
hicho kuhusu mikakati ya Jeshi la Polisi dhidi ya vyama vya siasa hasa
cha Cuf. Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Ulinzi Taifa, Mustafa Wandu na
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Zanzibar, Nassor Ahmed
Mazrul.
Na Dotto Mwaibale
MKURUGENZI
wa Uchaguzi wa Chama cha Wananchi (CUF) Shaweji Mketo amesema iwapo
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Ernest Mangu ataendelea kukifuatilia
chama hicho wanachama wa chama hicho watekwenda ofisini kwake
kumsalimia.
Mketo ameyasema hayo Makao Makuu ya Chama hicho Buguruni jana Dar es Salaam leo wakati Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrul alipo kuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu msimamo wa chama hicho kuhusu mikakati ya Jeshi la Polisi dhidi ya vyama vya siasa hasa cha Cuf.
“Tunasema sisi Cuf hatumuogopi IGP na kama ataendelea kutufuatafuata haita pita wiki mbili tutamfuata kwenda kumsalimia ofisi kwake” alisema Mketo. Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrul
alisema chama hicho kimesikitishwa na kauli ya IGP aliyoitoa hivi karibuni wakati akihojiwa Tido Mhando wa Kituo cha Televisheni cha Azzam kuwa jeshi hilo wakati wowote litamkamata Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad kwa kuwachochea wafuasi wake ili waichukie serikali iliyopo madarakani.
Alisema baada ya kuitafakari kauli hiyo ya IGP wamebaini kwamba hivi sasa IGP Mangu ameamua kuwathibitishia watanzania kuwa jeshi la polisi ni idara maalumu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Mazrul alisema kwa muda mrefu IGP Mangu amekuwa akilitumia jeshi la polisi kushiriki katika matukio mbalimbali ya kuhujumu demokrasia na kukiuka haki za binadamu kwa lengo la kukinusuru Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutokana na anguko kubwa la kukataliwa na wananchi kama ilivyothibitika kabnla na baada ya uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25 mwaka jana.
Alisema jeshi la polisi limekuwa na utaratibu wa kukamata raia, kuwapiga kuwabambikia kesi, kuwashikilia na kuwatesa katika vituo vya polisi bila ya kuwafikisha mahakamani.
Mazrul alisema hadi sasa zaidi ya wananchi 400 wameathiriwa kutokana na hujuma za jeshi la polisi kwa kuwabambikia kesi. (P.T)

SHARE
No comments:
Post a Comment