Kijana
Petro Magoti kutoka Shirikisho la Vyuo vya Elimu ya Juu-CCM, aliyeko
Ujerumani kwa masomo ya Uongozi na Uhusiano wa Kimataifa, akiagana na
mmoja wa wamiliki wa viwanda vikubwa Duniani, Prof. Karl Knoop, baada ya
kuzungumza naye, mjini Berlin, Ujerumani, juzi. Kushoto ni Meya wa
mji wa Bugermeister, David Osthotlhoff.
*NI PETRO MAGOTI
*AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA BILLIONEA KNOOP, NCHINI HUMO
*AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA BILLIONEA KNOOP, NCHINI HUMO
NA BASHIR NKOROMO
Katika kutekeleza azma ya Serikali ya awamu ya tano ya kuifikisha Tanzania katika mapinduzi ya viwanda vikubwa na Vidogo, Kijana Petro Magoti ambaye ni mwakilishi pekee kwa Tanzania aliyeko nchini Ujerumani, kwenye mafunzo ya uongozi na uhusiano wa kimataifa, amekutana na mmoja wa wamiliki wa viwanda vikubwa Duniani, Prof. Karl Heinz Knoop na kufanya mazungumzo naye ili kumshawishi kuja kuwekeza nchini.

Akizungumza
kutoka nchini Ujerumani, Magoti amesema leo kwamba, Prof. Knoop ambaye
anamiliki viwanda katika nchi 17 Barani Ulaya na katika nchi nne katika
bara la Afrika, katika mazungumzo yao, Prof. Knoop ameonyesha dhamira ya
kuwekeza Tanzania katika meneo ya Himo mkoani Kilimanjaro na Kilindi
mkoani Tanga.
Magoti
amesema, Prof, Knoop, amefikia dhamira hiyo baada ya kumweleza kwa kina
fursa za kiuchumi zilizopo Tanzania, na namna nchi ilivyojipanga
kuwapokea kwa ukarimu wawekezaji kutoka nchi za nje ikiwemo Ujerumani,
lengo likiwa kuifikisha nchi kuwa yenye viwanda na hivyo kuwezesha
wananchi wengi wakiwemo vijana kupata ajira za uhakika.
“Katika
mazungumzo yetu, Prof. Karl Heinz Knoop ameeleza kuwa na dhamira ya
kuwekeza Tanzania ili kuunga mkono juhudi za serikali za kuondoa
umasikini, hata hivyo akasema, awali amewahi kuonyesha azma hiyo kwa
wakati, lakini akakumbana na changamoto lukuki ikiwemo kupewa eneo la
kujenga viwanda vikubwa vya mashine za kilimo kama vile Matrektar,
Mashine za kupanda mbegu, Kuvuna na kukausha mazao, na Maghala makubwa
ya kuhifadhia vyakula na kiwanda cha magari makubwa ya mizigo”, aalisema
Petro.
Alisema,
katika mazungumzo yao, alimsihi na kumwomba Billionea huyo, Prof.
Knoop, kutokata tamaa katika dhamira yake hiyo ya kujenga viwanda
Tanzania kutokana changamoto ya awali aliykumbana nayo ya kupata eneo la
uwekezaji, badala yake afike Tanzania ili kuonana na Rais John Magufuli
ambaye kwake viwanda ni kipaumbele kikubwa.
“Nilimweleza
kuwa Mh. Rais wa Tanzania Dk. John Magufuli, anavutiwa saa na
wawekezaji walio tayari kuijenga Tanzania ya viwanda ili kukuza Uchumi
na kupunguza tatizo la ajira hasa kwa Vijana ambalo sasa ni kubwa zaidi
kuliko ilivyokuwa hapo awali, lakini nikamshauri pia Billionea huyo kuwa
akifika nchini kwetu, aombe kujenga viwanda vyake katika mikoa ya
Iringa na Morogoro ambayo kwa kuwa mikoa hiyo ina maeneo mengi na mazuri
kwa Kilimo.”, Magoti alisema Magoti na kuongeza,
“Baada ya
mazungumzo yetu tumekubaliana kwamba kati ya tarehe 17 hadi 22 Oktoba,
mwaka huu, Bilionea huyo atafika Tanzania kwa ajili ya kuonana na Mh.
Rais ili kujadiliana nae juu ya uwekezaji huo wa viwanda na ameahidi
kutembelea mikoa ya Iringa na Morogoro ili kujiridhisha na maeneo
yalivyo kwa ajili ya Uwekezaji katika Viwanda vya Kilimo.
Katika kuhakikisha kuwa fursa ya yeye kuwa nchini Ujerumani, anaitumia vilivyo kwa manufaa ya taifa, Magoti alitafuta nafasi na hatimaye akaipata ya kukutana na Wabunge wastaafu na viongozi mbali mbali wa Serikali ya Ujerumani wakiongozwa na Prof. Hemker anaetokana na Chama cha SPD.

Katika
yake na viongozi hao kutoka Kada mbali mbali Nchini Ujerumani wengi wao
wamekubali na kuahidi kuwa wako tayari kumuunga mkono Rais wa Dk. John
Magufuli katika azma yake ya kuijenga Tanzania yenye viwanda vingi, na
hivyo wameahidi kuja Tanzania kujenga viwanda vya kutengeneza mashine za
aina mbalimbali hususan za kilimo.
Magoti ambaye anatoka katika Shirikisho la Vyuo vya Elimu ya Juu-CCM, yupo Berlin, nchini Ujerumani kwa wiki ya pili sasa, akiendelea na masomo ya Uongozi na Uhusiano wa Kimataifa.(P.T)
Magoti ambaye anatoka katika Shirikisho la Vyuo vya Elimu ya Juu-CCM, yupo Berlin, nchini Ujerumani kwa wiki ya pili sasa, akiendelea na masomo ya Uongozi na Uhusiano wa Kimataifa.(P.T)
SHARE

No comments:
Post a Comment