
Na Khadija Khamis –Maelezo Zanzibar
Naibu
Waziri wa Afya Harusi Said Suleiman amesema hapendelei kuona wauguzi
wanatumbuliwa majipu kutokana na uzembe wao lakini hayuko tayari
kutumbuliwa yeye kwa ajili yao .
Hayo
aliyasema wakati alipokuwa akifanya ziara ya kutembelea vituo mbali
mbali vya Afya Wilaya ya Kaskazini B Unguja vikiwemo Kituo cha
Kiwengwa na Kituo cha Bubwini Misufini kutaka kuona changamoto zinazopo
vituo hapo.
Alisema
kuna baadhi ya wauguzi huwafanyia dharau wagonjwa au wajawazito wakati
wa kujifungua jambo ambalo halipaswi kuona linafanyika, kitu ambacho
kinaweza kuwapeleka pabaya na kutumbuliwa majibu.
“Sitoona
vizuri kuona mfanyakazi anatumbuliwa jipu kwa ajili ya uzembe wake na
pia siko tayari kutumbuliwa mimi kwa ajili yake “Alisema Harusi .
Aidha
alisema kwamba wauguzi wawetayari kukamilisha majukumu yao ya kikazi na
waache lugha chafu ambazo zitawasumbuwa wagonjwa na kuonekana kuwa wao
wakorofu katika kutoa huduma .
Hata
hivyo Naibu Waziri alieleza kuwa wauguzi waelewe kuwa awamu iliopo hivi
sasa ni awamu ya uwajibikaji na ufatiliaji na ni rahisi mawasiliano
kufika kwa haraka na kuweza kuharibu malengo ya baadae hivyo wasiwe
tayari kuchokozwa wakachokozeka.
Nae
Muuguzi wa kituo cha afya cha Kiwengwa Khadija Ali Juma alieleza
matatizo mbali mbali ambayo wanakabiliana nayo kituoni hapo ikiwemo
kutokuwa na uzio katika eneo hilo, wananchi kuchafua katika kwa makusudi
katika maeneo ya vyoo pamoja na kufanya maskani katika kituo hicho .
Aidha
alisema kutokuwa na friji katika kituo hicho kunachagia usumbufu mkubwa
wa kuhifadhia dawa za chanjo za mama na watoto ambazo zinahitajika
kuhifadhiwa katika sehemu yenye ubaridi ili zisiharibike .
Alisema
ushirikiano mdogo uliopo baina ya kituo cha afya na kamati ya sheha
hawaufurahikii wauguzi ,kwani sheha wa sehemu hiyo haonyeshi
ushirikiano mzuri na wauguzi waliopo katika kituo hicho .
Wakati
huo huo Naibu Waziri wa Afya alitembelea katika Kituo cha Afya cha
Bumbuni Misufini ambacho kilitokezea matatizo ya kutofahamiana kati ya
Wauguzi wa serikali na Wakunga wa Jadi .
aliwataka
wauguzi ambao ni waajiriwa wa serikali kutoa mashirikiano ya pamoja na
wakunga wa jadi ili kuepusha tofauti miongoni mwao na kuweza kutatua
changamoto ambazo zitaweza kujitokeza kwa wazazi.(P.T)
SHARE








No comments:
Post a Comment