Waziri wa
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema
mayai ya kuku wa kisasa yanayotengenezwa nchini yamedaiwa kuwa na
mabaki ya dawa ambazo ni hatari kwa afya ya binadamu.
Akizungumza
leo wakati alipozindua bodi mpya ya ushauri ya wizara kwa Mamlaka ya
Chakula na Dawa(TFDA), Mwalimu amesema amehakikishiwa na wataalamu hao
kuwa dawa zinazotumika kwenye mayai na kuku hao zinabaki ambapo si
salama kwa afya ya binadamu.
Mwalimu
amesema kutokana na dawa hizo kubaki kwenye mayai na kuku hao ameitaka
TFDA kufanya utafiti ili kujua kiwango kipi cha dawa zilizopo ili
Serikali iweze kuchukua hatua za haraka.
“Hivyo
tuwaachie TFDA waendelee na utafiti wao na wanapobaini ni kiasi gani cha
dawa zilizomo kwenye mayai na kuku hao watuambie haraka dawa zipi
hazitakiwi na zipi zinatakiwa ili kulinda soko la ndani,”amesema.
Pia
amewatahadhalisha wataalamu wa TFDA wasihofie kutoa majibu haraka kwa
kufikiri kuwa watakwamisha soko la ndani hivyo wanatakiwa wawe wa kweli
ili tatizo lililopo liweze kupunguzwa.
SHARE
No comments:
Post a Comment