Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
MKUU wa
Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kuwa suala la walimu wa
serikali kusafiri bure zinaendelea mpaka vyombo vyote vya usafiri
kukubali kufanya hivyo.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Makonda amesema walimu
lazma warahisishiwe maisha katika utendaji wao kazi ikiwa ni kupata
usafiri bure katika vyombo vya usafiri vilivyopo jijini Dar es Salaam.
Amesema
kuwa katika maombi yake walimu watasafiri bure katika usafiri wa gari
moshi za Pungu -Stesheni na Ubungo -Stesheni kwa kutumia vitambulisho
ambavyo viko katika utaratibi wa daladala.
Makonda
amesema kuwa ameomba Waziri wa Tamisemi juu ya walimu kusafiri bure wa
mabasi ya mwendo haraka na baada ya hapo kazi ya kupigania walimu katika
vyombo vyote usafiri ili waweze kufundisha watoto na wawe na viwango
vya juu vya ufaulu kuzidi mikoa yete nchini.
Aidha
amesema kuwa haitakuwa busara suala la walimu kusafiri bure haliwezi
likaachwa bila kuwa ufumbuzi kutokana kuamini kuwa walimu wakipata
usafiri wanaweza kufika mapema shuleni na kufundisha.
Nae
Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa TRL, Masanja Kadogosa amesema kuwa wanaunga
mkono jitihada za Rais katika elimu na kama taasisi ya serikali
wanachokufanya katika ysafiishaji wa walimu.
Kadogosa
amesema kuwa kama kampuni wamechelewa sana kuanza kutoa huduma hiyo na
kuongeza kuwa kwa wanafunzi watatumia usafiri huo kwa kulipa sh.100. (P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment