Naibu
Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za
Mitaa(Tamisemi)Suleimani Jaffo akizungumza wakati akifungua mafunzo ya
kusimamia na kutumia mitambo na magari ya kisasa ya kukusanya Taka ngumu
kwenye majiji na halmashauri zilizopo kwenye mpango wa kuendeleza miji
kimkakati unaosimamiwa na Ofisi ya Rais kwa mkopo kutoka Benki ya
Dunia,kushoto ni Mratibu wa Mradi huo,Mhandisi Davis Shemangale na kulia
ni Mkuu wa wilaya ya Arusha,Mrisho Gambo.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya usimamizi miundombinu ya ukusanyaji Taka ngumu wakimsikiliza Naibu Waziri,Suleimani Jaffo.
Naibu
Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za
Mitaa(Tamisemi)Suleimani Jaffo(aliyevaa tai nyekundu) akiwa ujumbe ofisi
yake na watumishi wa halmashauri ya Jiji la Arusha wakati akikagua eneo
lililotengwa kwaajili ya kuchomea taka ngumu lilipo Dampo Kuu jijini
humo katika mpango wa kuendeleza miji kimkakati unaosimamiwa na Ofisi ya
Rais.
Naibu
Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za
Mitaa(Tamisemi)Suleimani Jaffo akikagua Dampo la Jiji la Arusha
liliboreshwa miundombinu yake kulia kwake ni Mkuu wa wilaya ya
Arusha,Mrisho Gambo.
Naibu
Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za
Mitaa(Tamisemi)Suleimani Jaffo akifafanua jambo kwa waandishi wa habari.
Sehemu ya magari maalumu yatakayohusika kukusanya Taka ngumu kutoka mitaa mbalimbali ya Jiji la Arusha.
Naibu
Waziri Jaffo alitaka mitambo hiyo itumike kwa malengo yaliyokusudiwa na
kufanyiwa matengenezo kila mara ili iwe endelevu na kuongeza kuwa
serikali imeshaweka mikakati ya miji yote kuwa misafi.
SHARE
No comments:
Post a Comment