Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi
Dkt. Aziz Mlima akiongea na wadau wa takwimu wakati wa uzinduzi wa
warsha ya kitaifa kuhusu mpango wa Takwimu za Malengo ya Milenia kwa
niaba ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi leo jijini Dar
es salaam. Warsha hiyo inashirikisha wadau wa ndani na nje ya nchi.
Mkurugenzi
Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dkt. Albina Chuwa akitoa taarifa ya
ofisi yake ilivyojipanga katika kusimamia takwimu za taifa wakati wa
uzinduzi wa warsha ya kitaifa kuhusu mpango wa Takwimu za Malengo ya
Milenia kwa niaba ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi
leo jijini Dar es salaam. Warsha hiyo inashirikisha wadau wa ndani na
nje ya nchi.
Mkurugenzi
Mkuu wa Ofisi ya Takwimu Afrika Kusini, Bw. Pali Lehohla akitoa maelezo
kuhusu ofisi yake inavyoshirikiana na wadau mbalimbali katika
kausimamia takwimu za taifa hilo wakati wa uzinduzi wa warsha ya kitaifa
kuhusu mpango wa Takwimu za Malengo ya Milenia kwa niaba ya Katibu Mkuu
Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi leo jijini Dar es salaam.
Washiriki
wa warsha wakifuatilia hotuba ya uzinduzi wa warsha ya kitaifa kuhusu
mpango wa Takwimu za Malengo ya Milenia kwa niaba ya Katibu Mkuu
Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi leo jijini Dar es salaam.
Washiriki
wa warsha wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu,
Dkt. Albina Chuwa alipokuwa akitoa taarifa ya ofisi yake wakati wa
uzinduzi wa warsha ya kitaifa kuhusu mpango wa Takwimu za Malengo ya
Milenia leo jijini Dar es salaam.
(picha na Eleuteri Mangi, MAELEZO)
Na May Simba na Eleuteri Mangi, MAELEZO
SERIKALI
kupitia Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) imezindua mpango wa kuboresha
matumizi ya takwimu sahihi katika kutekeleza malengo 17 ya dunia kwa
maendeleo ya nchi.
Akizungumza
na wadau wa takwimu jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa warsha
ya kitaifa kuhusu mpango wa Takwimu za Malengo ya Milenia kwa niaba ya
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi, Katibu Mkuu Wizara ya
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Aziz Mlima
amesema kuwa matumizi ya takwimu sahihi yataisaidia Serikali kutekeleza
sera na mingo ya ili kutatua changamoto zinazowakabili wananchi.
Malengo
hayo ni pamoja na kutokomeza umasikini, njaa, kuimarisha afya na
ustawi, Elimu bora, usawa wa jinsia, maji safi na salama, nishati
mbadala kwa gharama nafuu, kazi zenye staha na ukuzaji uchumi, viwanda,
ubunifu na miundombinu, na jamii endelevu.
Malengo
mengine ni matumizi na uzalishajinwenye uwajibikaji, kuchukua hatua
dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi, kuendeleza uhai katika maji, kulinda
uhai katika ardhi, amani, haki na taasisi madhubuti pamoja na
ushirikiano ili kufanikisha malengo.
Dkt.
Mlima amesema kuwa mpango huo uliozinduliwa utaisaidia Tanzania kufikia
malengo ya maendeleo endelevu kulingana na Mpango wa Maendeleo wa Taifa
wa mwaka 2025.
Aidha,
Serikali inaendelea kusimamia kuwekeza zaidi katika ukusanyaji wa
takwimu sahihi kwa lengo la kuweka, kufuatilia na kutekeleza mipango
yake kwa kulingana na malengo iliyojiwekea.
“Hatua
hii itasaidia kuendeleza malengo ya SDG kupitia upatikanaji wa takwimu
kwa njia ya uwazi ambayo itakuwa ya haraka kutuonyesha mapungufu na
hivyo kutatua changamoto zinazoikabili jamii” Dkt. Mlima
Dkt.
Mlima amezitaka Wizara, Taasisi na Mashirika mbalimbali kuendelea
kushirikiana ili kuhakikisha uwepo wa usimamizi thabiti katika kupima
matarajio ya maendeleo yanayokusudiwa.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dkt. Albina
Chuwa amesema kuwa lengo la warsha hiyo ni kuja na mipango ambayo
itahusisha matumizi sahihi ya takwimu zitakazoisaida Serikali kutatua
changamoto zilizopo na kutoa mwelekeo katika kutekeleza sera za nchi.
Vilevile,
Dkt. Albina amesema kuwa, mpango huo utahusisha wadau mbalimbali wa
ndani na nje ya nchi ambapo wamependekeza kuwepo kwa kamati
itakayohusisha viongozi wa juu wa Serikali na kusimamiwa na Ofisi ya
Waziri Mkuu au Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi kwa kuwa wapo kwenye ngazi
ya maamuzi.
Naye
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Takwimu Afrika Kusini, Bw. Pali Lehohla
amesema kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazofanya vizuri katika
suala la takwimu na kushauri mataifa mengine ya Afrika kujifunza namna
Ofisi ya Taifa ya Takwimu inavyopaswa kuongozwa na uongozi bora na
imara.
MWISHO
SHARE
No comments:
Post a Comment