Wananchi
wa Zambia wanasubiri matokeo ya awali ya uchaguzi mkuu ambao unatajwa
kuwa ulikuwa wa ushindani mkubwa baina ya Rais Edgar Lungu na mpinzani
wake wa karibu Hakainde Hichilema, anayemtuhumu kwa kushindwa kuimarisha
uchumi wa taifa hilo.
Rais
Lungu ambaye alimshinda mpinzani wake kwa idadi ndogo ya kura katika
uchaguzi wa mwaka jana, baada ya kifo cha mtangulizi wake Michael Sata,
huenda akalazimika kuingia kwenye duru ya pili ya uchaguzi ikiwa
hatapata nusu ya kura.
Licha ya
kuwa matokeo rasmi ya awali bado hayajaanza kutolewa, maofisa wa tume ya
uchaguzi wa Zambia, wanasema kuwa maelfu ya raia walijitokeza kushiriki
kupiga kura kwenye uchaguzi wa Alhamisi, Agosti 11.
Uchumi wa
taifa la pili kwa uzalishaji wa shaba, liko kwenye shinikizo kubwa
kutokana na kupanda kwa gharama za usafirishaji wa madini hayo, huku
Serikali ikijaribu kulishawishi shirika la fedha duniani IMF kuisaidia
kifedha.
Wakati wa
kampeni wafuasi wa chama tawala cha PF cha Rais Lungu walikabiliana
mara kwa mara na wale wa kiongozi wa upinzani wa chama cha UPND,
Hichilema, lakini hakukuripotiwa vutugu zozote wakati wa zoezi la
upigaji kura.
Ikiwa
matokeo hayatatoa mshindi aliyefikisha zaidi ya asilimia 50, badi huenda
wagombea wawili waliopata alama za juu watachuana kweye duru ya pili
ndani ya siku 37.
Hichilema
ambaye ni mfanyabiashara na mtaalamu wa masuala ya uchumi, amesema yeye
ndiye mgombea pekee anayefuzu zaidi ya Lungu kuongoza taifa taifa hilo.
Hata hivyo Rais Lungu mwenyewe anasema anahitaji muda zaidi wa kuwatumikia wananchi wa Zambia.
Tume ya
uchaguzi ya Zambia yenyewe inasema itatangaza matokeo rasmi ya uchaguzi
huu, Jumamosi jioni au mapema siku ya Jumapili mara baada ya zoezi la
kuhesabu kura kukamilika.RFI
SHARE
No comments:
Post a Comment