Makamu
Mwenyekiti wa Kamati ya Baraza la Vyama vya Siasa, Bw.Vuai Ali Vuai
akizungumza na Wajumbe wa Kamati (hawapo pichani) wakati wa kikao cha
dharura cha Kamati ya Uongozi ya Baraza.
Bw.Constantine B. Akitanda, Mjumbe wa Kamati ya Baraza la Vyama vya Siasa akisisitiza jambo wakati wa kikao hicho.
Wajumbe
wa Baraza la Vyama vya Siasa wakati wa kikao cha dharura cha Kamati ya
Uongozi wa Baraza hilo kilichokutana kujadili hali ya siasa Jijini Dar
es Salaam.
Na Monica Laurent, Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa
Wajumbe wa Kamati ya Uongozi ya Baraza la Vyama vya Siasa wamekutana jana Jijini Dar es Salaam kujadili hali ya Siasa nchini.
Katika
kikao hicho ambacho kilikuwa cha dharura kilichofanyika katika ukumbi
wa mikutano wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ,wajumbe
wamekubaliana kwa pamoja kuwa, ipo haja ya kuitishwa kwa kikao cha
Baraza la Vyama vya Siasa kujadili hali ya siasa nchini.
Akizungumza
wakati wa kikao hicho Bw. Vuai Ali Vua ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa
Baraza la Vyama vya Siasa amesisitiza kuwa Kamati ya Uongozi inalo
jukumu la kuimarisaha na kudumisha hali ya amani nchini pamoja na
kujadili changamoto zilizopo katika mfumo wa demokrasia ya vyama vingi .
Aidha,
wajumbe wa kikao cha Kamati ya Uongozi wameazimia kuonana na Waziri
Mkuu, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa kwa lengo la kujitambulisha,
kuelezea umuhimu wa Baraza la Vyama vya siasa katika mfumo wa vyama
vingi na kubadilishana mawazo kuhusu hali ya siasa nchini.
Kamati ya
Baraza la Vyama vya Siasa huundwa na Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti
wa Baraza ambao huchaguliwa na wajumbe wa Baraza, Katibu wa Baraza akiwa
ni Msajili wa Vyama vya Siasa ambaye yuko kisheria na pia wenyeviti wa
kamati nne za Baraza. (P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment