
Na Is-haka Omar, Zanzibar.
CHAMA cha
Mapinduzi (CCM) Zanzibar kimeipongeza hotuba ya Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzanzia Dkt. John Pombe Magufuli aliyotoa katika ziara
zake Zanzibar, iliyosisitiza dhamira ya serikali kuharakisha maendeleo
kwa wananchi bila ya kujali tofauti za kisiasa.
CCM
imesema inaunga mkono na kupongeza kwa dhati hotuba hizo zilizotolewa
Unguja na Pemba ziliyosisitiza dhamira ya serikali zote mbili ya jamhuri
ya muungano wa Tanzania na Zanzibar kuwaletea wananchi maendeleo bila
ya kujali itikadi za kisiasa.
Akizungumza
Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar wa Idara ya ya Itikadi na
Uenezi, Waride Bakari Jabu alisema viongozi na wananchi kwa ujumla
wanatakiwa kushirikiana katika ujenzi wa maendeleo ya nchi ili zanzibar
iweze kufikia hadhi ya kuwa nchi yenye uchumi mkubwa katika nchi za
Afrika.
Waride
alieleza kwamba ziara hiyo imetoa muongozo imara wa kuwakumbusha
watendaji na viongozi nchini juu ya dhamana na mambo ya msingi
wanayotakiwa kuyatekeleza kwa wananchi.
“CCM
tunaunga mkono kwa nguvu zote hotuba ya Rais wetu Dkt. John Magufuli
kwani imezungumzia na kugusia mambo ya msingi yanayogusa maisha ya
wananchi hasa wa kipato cha chini na kutoa muongozo wa namna gani
serikali zetu zinaendelea na mikakati imara ya kuimarisha uchumi na
maendeleo ya nchi kwa ujumla.
Pia
tunatakiwa kuendelea kuwa wamoja na wazalendo bila ya kujali tofauti
zetu za kidini, kisiasa na kikabila kwa kulinda amani na utulivu wa nchi
zetu kwani ndio siri ya mafanikio ya nchi zetu.”, Alisisitiza Waride.
Katibu
huyo , alisema Dkt. Magufuli ameonyesha nia ya dhati ya kuendelea
kutafuta fursa mbali mbali za miradi ya maendeleo itakayoweza
kuharakisha maendeleo ya Zanzibar.
Alisema
miongozo mwa mambo ya msingi yaliyosisitizwa na Dkt. Magufuli pia
yanaungwa mkono na CCM Zanzibar ni dhamira ya kuhakikisha Zanzibar
inakuwa ni nchi ya Viwanda vya kusindika samaki wanaotokana na Uvuvi wa
Kisasa wa Bahari kuu vitakavyotoa fursa za ajira kwa vijana na wananchi.
Waride,
alipongeza juhudi zinazofanywa na Serikali ya Muungano wa Tanzania kwa
kufungua milango ya wawekezaji wakubwa kuwekeza Zanzibar huku wakitafuta
wahisani kutoa mamilioni ya fedha za kuendesha miradi ya kijamii
ukiwemo mradi wa maji safi Unguja uliotolewa fedha za mkopo na Serikali
ya India.
Alisema
kwa ushirikiano wa Rais Dkt. Magufuli na Dkt. Shein, CCM inaamini kwamba
Tanzania bara na Zanzibar kwa ujumla zitakuwa nchi za kupigiwa mfano
duniani katika nyanja mbali mbali za kimaendeleo, kisiasa na kijamii.
Alifafanua
kwamba CCM Zanzibar, inaungana na Dkt. Magufuli kupinga siasa za
misimamo mikali na utengano zinazofanywa na baadhi ya vyama vya kisiasa
Zanzibar kuwa haziwezi kuleta maendeleo ya nchi badala yake zitajenga
migogoro isiyokuwa ya lazima.
Alisema
CCM inasifu msimamo wa Dkt. Magufuli wa kulinda Muungano na Mapinduzi ya
Zanzibar ya Mwaka 1964 huku akiahidi kuendelea kulinda amani na Utulivu
wa nchi kwa gharama yoyote.
Pamoja na
hayo Waride aliahidi kuwa CCM itaendelea kuwa balozi mzuri wa kuwasihi
wafuasi wa chama hicho na wananchi kwa ujumla kufanya siasa za maendeleo
zitakazoweza kwenda sambamba na malengo ya serikali.
Aidha
Waride alipongeza juhudi za Rais wa Zanzibar, Dkt. Shein za kuongoza
nchi kwa ufanisi mkubwa licha ya kuwepo na changamoto mbali mbali za
kisiasa nchini.
Alielezea
kuridhishwa kwake na kauli ya Dkt. Shein ya kuwataka wapinzani kusahau
Serikali ya Mpito kama inavyodaiwa na baadhi ya viongozi huku
akisisitiza hakuna sababu ya kuwa na aina ya serikali hiyo kwa sababu
uchaguzi umefanyika kwa njia ya huru na haki.
Katika
Mkutano huo, Dk Shein alisema kazi kubwa inayofanywa kwa sasa ni
kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2015, huku Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar ikiwa katika hatua ya mwisho ya kuanza kazi za
kuchimba mafuta na ges ili kutoa hatua pana ya ajira kwa wananchi.
Alisema
muswada wa mafuta na gesi tayari umewasilishwa katika Baraza la
Wawakilishi na kusomwa kwa mara ya kwanza ambapo katika kikao kijacho
cha Baraza la Wawakilishi kitakachofanyika Septemba 26 utasomwa kwa mara
ya pili na kusubiri saini yake.
Ziara
hiyo ya Dkt. Magufuli ya kuwashukru wananchi wa Zanzibar kwa kumchagua
kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uchaguzi Mkuu
uliopita, imefanyika katika maeneo mbali mbali Pemba na Unguja. (P.T)
SHARE








No comments:
Post a Comment