Chama cha
Kansela Angela Merkel wa Ujerumani cha Christian Democratic CDU
kimepoteza nafasi yake kama chama cha pili chenye nguvu katika uchaguzi
wa Mecklenburg-Vorpommern uliofanyika siku ya Jumapili.
Kwa
mujibu wa matokeo rasmi ya uchaguzi yaliyotolewa chama kinachopinga
wahamiaji cha mbadala kwa Ujerumani AfD, kimeibuka nafasi ya pili.
AfD
imepata kura asilimia 20.8, ikimaniisha kwamba chama hicho kitaingia
bunge la jimbo hilo la kaskazini mashariki kwa mara ya kwanza. Tayari
kimeshapata wawakilishi katika majimbo mengine nane na hii ikiashiria
kwamba kinaweza kuingia katika bunge la taifa baada ya uchaguzi mkuu wa
mwakani. CDU imeibuka na asilimia 19 ya kura zilizopigwa katika uchaguzi
huo uliotabiriwa kwa kiwango kikubwa kuwa ungekuwa ni mtihani mpya kwa
sera za Bi. Merkel zenye utata kuhusu mgogoro wa wakimbizi.
Chama cha
siasa za wastani za mrengo wa kushoto cha Social Democratic SPD ambacho
kwa hivi sasa kinaongoza Muungano mkuu na CDU kama mshirika wake mdogo,
kimesalia kuwa chama chenye nguvu baada ya kupata asilimia 30.6.
Matokeo yanamaanisha kwamba, licha ya vyama vyote ambayvo vinaongoza
serikali kupoteza, SPD na CDU bado vitaweza kuunda Muungano kwa kipindi
cha miaka mitano. Ingawa mshindi wa uchaguzi huo kutoka chama cha SPD
Erwin Sellering hajasema ikiwa atataka kuungana tena na CDU.
Sera ya wakimbizi yachangia
Kiongozi
wa chama cha AfD Frauke Petry amesema mafanikio waliyoyapata katika
uchaguzi huo wa jimbo la Mecklenburg-Vorpommern ambalo ni nyumbani kwa
jimbo la uchaguzi la Kansela Merkel la Stralsund, ni matokeo ya "janga
la sera ya wakimbizi" akiongeza kwamba "tumeiweka CDU sehemu
inakostahili".
Katibu
mkuu wa CDU Peter Tauber amesema kuanguka kwa chama chao kumetokea kwa
sababu kumekuwa na ongezeko la "kutoridhishwa na upinzani" dhidi ya
uamuzi wa Merkel wa kutoifunga mipaka ya Ujerumani dhidi ya wakimbizi.
Matokeo
hayo pia yameashiria ukweli kwamba AfD imegawana kura miongoni mwa vyama
na kwamba asilimia 34 ya wafuasi wake hawakupiga kura katika uchaguzi
uliopita wa mwaka 2011. Uungwaji mkono wa umma kwa bi Merkel ulishuka
wakati wa mashambulizi mawili ya kigaidi ya mwezi Julai yaliyotekelezwa
na waomba hifadhi na kudaiwa kufanywa na kundi linalojiita dola la
Kiislamu IS. Wakosoaji wa uamuzi wake wa kutofunga mipaka ya Ujerumani
ambao ulishuhudia kuwasili kwa wakimbizi milioni 1.1 kwa mwaka 2015,
wanasema Merkel ni wa kulaumiwa kwa kuleta kitisho cha usalama nchini
Ujerumani.
Mwanachama
mmoja wa CDU Klaus Dieter Arlt amesema matokeo haya waliyatarjia.
"Matokeo haya hayashangazi bali yanakatisha tamaa. Yamedhihirisha kuwa
vyama vikuu viwili, CDU na SPD havijaweza kutatua matatizo ya watu".
Kwa
mujibu wa utafiti uliofanywa kabla ya uchaguzi na Infratest Dimap, zaidi
ya theluthi tatu ya wapiga kura wa Mecklenburg-Vorpommern walisema
kwamba utitiri wa wakimbzii ungekuwa ni kigezo cha maamuzi siku ya
upigaji kura. DW
SHARE
No comments:
Post a Comment