
Chama Cha
Wananchi CUF leo kipitia mkutano wake na wanahabari kimejibu kauli
zilizotolewa na Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli alizozitoa
juzi na jana (tarehe 2-3/9/2016) katika mikutano ya hadhara aliyoifanya
katika kisiwa cha Pemba, Uwanja wa Gombani na Unguja katika Uwanja wa
Demokrasia (Kibandamaiti).
Soma taarifa yao hapa chini;
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Waheshimiwa wanahabari,
Awali
napenda kuchukua fursa hii kuwashukuru kwa kuitikia wito wetu,
nawapongeza kwa kazi nzuri mnayoendelea kuifanya ya kutupasha habari
mbalimbali zinazohusiana na hali ya kisiasa, kiuchumi na kijamii ndani
ya nchi yetu na nje ya mipaka yake. Lakini pia kuwapa pole kutokana na
namna mnavyotekeleza majukumu yenu katika mazingira magumu ya hofu na
vitisho vinavyofanywa na watendaji wa serikali ya awamu ya tano. Nitumie
fursa hii pia kwa kuwa ni mara yangu ya kwanza rasmi kuzungumza na
vyombo vya habari toka BARAZA KUU LA UONGOZI CUF TAIFA liniamini na
kunipa dhamana kubwa ya utendaji na usimamizi wa chama chetu kwa
kuniteua kuwa MWENYEKITI WA KAMATI YA UONGOZI WA CHAMA CHETU CHA
WANANCHI CUF TAIFA, tukisimamia majukumu yaliyopaswa kufanywa na
Mwenyekiti wa Chama Taifa na Makamu Mwenyekiti Taifa. Naahidi
nitatekeleza wajibu wangu kwa uaminifu mkubwa na weledi wa hali ya juu
kwa madhumuni ya kuwaletea watanzania mabadiliko sahihi ya maendeleo ya
kisiasa na kiuchumi wanayoyataka katika Taifa letu.
Waheshimiwa wanahabari,
Tumewaiteni
na kuomba kuzungumza nanyi kwa lengo la kujibu kauli zilizotolewa na
Mwenyekiti wa CCM, Rais John Magufuli alizozitoa juzi na jana (tarehe
2-3/9/2016) katika mikutano ya hadhara aliyoifanya katika kisiwa cha
Pemba, uwanja wa Gombani na Unguja katika uwanja wa demokrasia
(Kibandamaiti) na kupitia nyinyi tufikishe ujumbe wetu kwa Mwenyekiti wa
CCM, Rais JOHN MAGUFULI na watanzania kwa ujumla. Mwenyekiti wa CCM,
Rais John Magufuli amezungumza mambo mengi na pia amejikita katika kutoa
kauli za dhihaka na mipasho dhidi ya Chama cha Wananchi CUF na katibu
mkuu wetu Maalim Seif Sharif Hamad jambo ambalo tunaamini kwa hadhi na
heshima ya nafasi yake na hadhi ya taasisi ya urais hakupaswa kufanya
hivyo kama kiongozi wa nchi. Pamoja na masuala mengine Mwenyekiti wa
CCM, Rais JOHN MAGUFULI amesema amekwenda kuwashukuru wananchi wa Unguja
na Pemba kwa kumchagua yeye pamoja na Dokta Ali Mohamed Shein,
amewahahakishia Wazanzibari kuwa atailinda amani ya nchi kwa nguvu zake
zote na yeyote atakayejaribu kuivuruga amani atamshughulikia kwa nguvu
zake zote bila huruma, ataulinda Muungano kwa nguvu zake zote na lazima
uendelee kudumu katika kipindi chote cha utawala wake. Tatu,
amezungumzia maendeleo – Maji, viwanda, miundombinu, uvuvi na kadhalika
lakini pia amezungumzia kuitunza amani akitolea mifano ya nchi
zisizokuwa na amani ikiwemo Libya, Iraq, Syria, Somalia na mauaji ya
kimbali yaliyotokea Rwanda mwaka 1994. Magufuli amepongeza aliyooiita
“kazi nzuri ya majeshi” nadhani kwa kuisaidia kupata ushindi na
kuwathibiti wanaotaka mabadiliko na amempongeza Jecha Salim Jecha,
Mwenyekiti wa ZEC, kwa kufuta uchaguzi wa tarehe 25/10/2016 uliompa
ushindi Maalim Seif Sharif Hamad, na kumuombea apewe tuzo kwa kazi nzuri
aliyoifanya. Anashangaa kwanini Dokta Shein ameunda serikali kwa
kuvishirikisha vyama vingine wakati alishinda (Shein) kwa asilimia 99
huku akijigamba kuwa yeye kamwe hawezi kuingiza na hataingiza mtu hata
mmoja kutoka upinzani katika serikali yake pamoja na kupata ushindi wa
asilimia 58 anasahau kuwa hivi karibuni amemteua Mwenyekiti wa TLP Mhe.
Agustino Lyatonga Mrema, kuwa Mwenyekiti wa bodi ya PAROLE.
MSIMAMO WA CUF JUU YA KAULI ALIZOZITOA RAIS MAGUFULI:
THE CIVIC
UNITED FRONT (CUF CHAMA CHA WANANCHI) kimesikitishwa na kauli zisizofaa
kwa heshima na hadhi ya taasisi ya urais na nafasi yake kama kiongozi
wa nchi kutoka kauli za uchochezi, kupandikiza chuki na uhasama,
kuwagawa wananchi na kutaka kujenga chama chake kwa njia ya vitisho na
kutumia vyombo vya dola. Tunamtaka Mwenyekiti wa CCM, Rais Magufuli
atambue kuwa hatoweza kujenga umoja wa watanzania kwa kutoa kauli za
kuimarisha chuki, uhasama na kutosimamia haki, na kuunga mkono vitendo
vya uvunjaji wa demokrasia na sheria za nchi. Rais Magufuli hawezi kuwa
mfano wa kuigwa kwa vizazi vijavyo katika mikakati ya mataifa masikini
ya kulinda sheria, haki za kiraia, utawala bora na kuleta maendeleo
shirikishi (Inclusive Develeopment).Kauli nyingi za kuchochea chuki na
uhasama alizozitoa Rais Magufuli si za kwanza wala si ngeni kwa
Wazanzibari. Kisiasa wazanzibar na hasa wafuasi wa CUF (ambao ni wengi)
wamekuwa waathirika wakubwa wa matumizi makubwa ya ukandamizaji na
unyanyasaji iunaofanywa kikatili sana kupitia MAJESHI, MAZOMBI,
JANJAWIDI nakadhalika. Mauaji yaliyofanywa na Serikali ya CCM chini ya
utawala wa serikali ya awamu ya Tatu iliyoongozwa na Benjamini William
Mkapa Januari 26-27, 2001
yalisababisha
watu 46 kuuliwa na vyombo vya Ulinzi, watu 38 wameuwawa kwa kificho
mpaka leo hawajaonekana. Watanzania 658 waliojeruhiwa, na 135 waliopata
vilema vya kudumu katika maisha yao. Aidha zaidi ya wazanzibar 4000
waliishi kama wakimbizi Shimoni, Mombasa nchini Kenya, orodha yao
tumeiambatanisha na taarifa hii. Kama kweli Rais Magufuli anataka
kulinda amani ya Tanzania haiwezekani kuwa raia wamekuwa wakipigwa na
kuteswa na kukatwa viungo vyao na kuporwa mali zao na vikosi vya
majeshi, Mazombi na akiwa kimya na kutoa kauli za kubariki vitendo
hivyo. Kwa mtizamo wa Magufuli, ukatili na uhuni unaotendwa na MAZOMBI
ukiungwa mkono na vikosi vya majeshi ya SMZ na vile vya Muungano eti
ndiyo ulinzi wa amani. Lakini, Kauli mfano wa hizi zimewahi kutolewa na
watangulizi wake na viongozi wa Zanzibar waliopita. Hata hivyo mwisho wa
yote hawakuweza kufanikiwa kuwahadaa wazanzibari kudai haki yao na
mwaka hadi mwaka wazanzibar wanaotaka mabadiliko wawekuwa wakiongezeka
na kuidhihirishia dunia kuwa hawawezi kuvunjwa moyo na vitisho, hujuma
na ukandamizaji.
Mwenyekiti
wa CCM, Rais John Magufuli amemsifia Dokta Ali Mohamed Shein kwa
kuchaguliwa kuwa Rais wazanzibar kwa kura nyingi. Jambo hili
linachekesha na kustaajabisha dunia, kwani Hata mtoto mdogo anayeishi
Zanzibar au Tanganyika anatambua kuwa Dr. Shein si rais halali wa
Zanzibar. Ni rais aliyeingizwa madarakani kwa kile kinachoweza kuitwa
“tyranny of the highest order of the African Power Mongers who are ready
to shed blood for power” yaani “udhalimu wa kiwango cha juu kabisa
kinachofanywa na viongozi waroho wa madaraka ambao wako tayari kumwaga
damu ili watawale”. Katika uchaguzi halali wa tarehe 25/10/2016.
Wazanzibar walimchagua kwa kura nyingi kabisa, Maalim Seif Sharif Hamad
kuwa Rais wao. Wazanzibari wanajua hivyo, Watanzania wanajua hivyo,
Waafrika wanajua hivyo na dunia inaimba wimbo huo. Kujidanganya kuwa
Dokta Shein ni rais halali wa Zanzibar ni uotaji wa ndoto ya mchana kuwa
Tanzania ina viwanda kila kata na kila kijiji, ndoto ambayo kwa aina ya
uongozi wa John Magufuli haiwezi kutimia.(P.T)
SHARE








No comments:
Post a Comment