
Séraphin Moundounga, Waziri wa Sheria wa Gabon. (Hapa ni mwezi Juni 2015 mjini Libreville).
Waziri wa
Sheria wa Gabon Seraphim Moundounga ametangaza Jumatatu hii mchana
kwenye vyombo vya habari mjini Libreville, uamuzi wake wa kujiuzulu.
Taarifa ambayo imethibitishwa na Waziri huyo kwa RFI.
"Baada
ya kuona kwamba upande wa utawala, hawakutoa jibu kuhusu wasiwasi wa
muhimu wa kupatikana kwa amani na kuendeleza demokrasia, nimeamua
kuchukua uamuzi wa kuchukua likizo, upande mmoja, katika chama cha
Democratic Party, na kuachana na majukumu yangu kama mjumbe wa serikali
na hasa kuachana na vitendo hivi vikuu viwili, ili niweze kuwa huru kwa
shughuli zagnu za kila siku. "
Hayo
yakijiri Ufaransa imesema "haina taarifa yoyote kuhusu waliko raia wake"
baada ya machafuko makubwa yaliyofuata tangazo la kuchaguliwa kwa mara
nyingine tena kwa Rais Ali Bongo nchini Gabon, Waziri wa Mambo ya Nje wa
Ufaransa, Jean-Marc Ayrault, amesema Jumatatu hii katika taarifa yake.
"Watu
wengi wamekua wakikamatwa katika siku za hivi karibuni. Ufaransa haina
taarifa yoyote kuhusu waliko raia wake, " amesema Waziri, ambaye
ameonyesha" wasiwasi wake mkubwa". Watu kadhaa, wenye uraia wa nchi
mbili Ufaransa na Gabon hawajulikani walipo, chanzo cha kidiplomasia
kumeliambia shirika la habari la AFP.
Vurugu
zilizuka nchini Gabon baada ya kutangazwa kuwa Ali Bongo Ondimba
ameshinda uchaguzi wa urais uliyofanyika wiki moja iliyopita. Upinzani
umeendelea kupinga matokeo yaliyotangazwa na Waziri wa Mambo ya Ndani
yanayompa ushindi Ali Bongo Ondimba.
Upinzani
umeendelea kudai kuhesabiwa upya kwa kura katika vituo vyote vya kura
vya mkoa wa Haut-Ogooué, ambako inadhaniwa kuwa kura ziliibwa.
Rais wa
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa mwezi huu, Balozi wa New
Zealand Gerard van Bohemen, aliwatolea wito "wagombea wote, wafuasi wao,
vyama vya siasa na wadau wengine kuwa watulivu, kukomesha vurugu au
uchochezi wowote na kutatua migogoro ya aina yoyote kwa njia ya
utaratibu wa kisheria na kikatiba. "
Machafuko nchini Gabon yamesababisha vifo vya watu zaidi ya saba na wengine wengi wamekamatwa na wengine hawajulikani waliko.RFI
SHARE
No comments:
Post a Comment