TRA

TRA

Tuesday, September 13, 2016

Jesse achaguliwa Mwenyekiti KIDIFA

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !


jes2
Mwenyekiti wa KIFIDA aliyemaliza muda wake, Hassan Ngubege akimkabidhi Mwenyekiti mpya wa chama hicho Jesse John katiba ya chama hicho.
Na Mwandishi Wetu,Kisarawe
MTANGAZAJI nguli wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Jesse John amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Kisarawe (KIDIFA) katika uchaguzi uliofanyika jana.
Jesse ambaye aliupata uongozi huo katika uchaguzi uliokuwa na ushindani mkubwa aliibuka kidedea baada ya kupata kura 32 na kumshinda mpinzani wake Karim Wenge aliyepata kura 21.
Katika uchaguzi huo Mohamed Lubondo alichaguliwa kuwa Katibu baada ya kupata kura 30 na kumshinda Francis Mkamba aliyepata kura 27.Katibu Msaidizi alichaguliwa kuwa Amosi Kisebengo, Makamu Mwenyekiti alichaguliwa kuwa Abdul Mogella.
Wasimamizi wa uchaguzi huo kutoka Chama Mpira wa Miguu Mkoa wa Pwani (COREFA), Mweka Hazina wa KIDIFA alichaguliwa Iddo Mtangaze na Mweka Hazina Msaidizi alichaguliwa kuwa Sadiki Nasoro.
Mwakilishi wa klabu kutoka Tarafa ya Mzenga alichaguliwa kuwa Suleiman Mahenge, kutoka Tarafa ya Sungwi alichaguliwa Abdallah Kuga na Mwakilishi wa klabu alichaguliwa kuwa Ally Madega na Mwakilishi wa Mkutano Mkuu wa mkoa alichaguliwa kuwa Mohamed Masenga.
Mwenyekiti wa KIDIFA aliyemaliza muda wake Hassan Ngubege akimkarisha Jesse kushukuru wajumbe aliwataka viongozi wapya kufufua matumaini ya vipaji vya vijana katika soka wilaya ya Kisarawe kwa kuanzisha mashindano mbalimbali yenye lengo la kutafuta vipaji.
Jesse akiwashukuru wajumbe hao aliahidi kushirikiana na wadau wa soka ndani na nje ya wilaya hiyo kupata timu ya wilaya itakayoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom kama timu nyingine zinashiriki mashindano hayo.
Mwenyekiti Jesse alisema wilaya ya Kisarawe ambako yeye ni mzaliwa wa asili alisema anaamini vijana wengi hawajapata nafasi ya kuonesha vipaji vyao hivyo atatumia miaka minne ya uongozi kuzalisha vijana wazuri katika soka. (P.T)

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger