TRA

TRA

Saturday, September 3, 2016

KIWANDA CHA SARUJI CHAIPIGA TAFU SHULE YA SEKONDARI YA ILBORU YA ARUSHA

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !


Mkuu wa Idara ya Rasilimawatu kiwanda cha Sauji cha Simba Cement cha Tanga, Diana Malambugi, akimkabidhi mifuko ya saruji 400 yenye thamani zaidi ya milioni 4.8 kwa mwalimu mkuu shule ya Sekondari ya Ilboru ya Arusha, Julias Shulla ikiwa ni ujenzi wa vyumba vya madarasa.nyuma kulia ni Mkuu wa fedha Pieter Jaggar na kushoto ni Emmanuel Jonas mhasibu.
Tanga, KIWANDA Cha Saruji Cha Simba (Simba Cement) cha Tanga, kimeipa shule ya Sekondari ya Ilboru Secondary School ya Arusha mifuko 400 ya saruji yenye thamani zaidi ya milioni 4.8 kwa ujenzi wa vymba vya madarasa.

Akizungumza wakati wa halfa fupi ya makabidhiano leo, Mkuu wa Idara ya Rasilimaliwatu kiwanda cha Saruji cha Simba Cement, Diana Malambugi, alisema msaada huo umetolewa ili kupunguza changamoto za vyumba vya madarasa kwa shule hiyo.

Alisema msaada huo utapunguza uhaba wa vyumba vya madarasa na kutoa wito kutumika kama ilivyokusudiwa na kuiagiza kamati ya shule kuhakikisha mifuko hiyo inatumika ipasavyo.

‘Mifuko hii ya saruji itapunguza changamoto inayoikabili shule yako ikiwemo vyumba vya madarasa na ujenzi wa nyumba za walimu, sera yetu moja wapo ni hii ya elimu” alisema Malambugi

Alimtaka mwalimu huyo na kamati yake ya shule kuitunza mifuko hiyo ya saruji na kumhakikishia kuisaidia pale ambapo kutakuwa na uhitaji na kuwataka wadau wengine wa elimu kusaidia sekta ya elimu zikiwemo kuondosha changamoto za uhaba wa madawati na vyumba vya madarasa.

Kwa upande wake, mwalimu mkuu wa shule ya Ilboru sekondari school , Julias Shulla, alikishukuru kiwanda hicho na kusema kuwa msaada huo utatumika kama ilivyoombwa.

Alisema shule yake inakabiliana na changamoto nyingi zikiwemo uhaba wa vyumba vya madarasa pamoja uhaba wa vifaa vya maabara hivyo kuwataka wadau wa elimu kuisaidia.

‘Tunakishukuru kiwanda cha saruji cha simba kwa moyo wao waliounyesha kwetu, kwa fadhila hii tunawaahidi kuwa tutaitumia saruji kama tulivyoiomba” alisema Shulla

Alisema mifuko hiyo itapunguza kwa kiasi kikubwa changamoto ambazo shule yake inakabiliana nazo na kusema kuwa msaada huo ni faraja kwao na wanafunzi wa shule yake.
Mhasibu wa kiwanda cha Saruji cha Simba Cement, Emmanuel Jonas, akimkabidhi mwalimu mkuu wa shule ya Sekondari ya Iboru ya Arusha, Julias Shulla mifuko ya saruji 400 yenye thamani zaidi ya shilingi milioni 4.8 kwa ajili ya ujenzi wa vymba vya madarasa, nyuma ni mkuu wa fedha, Pieter Jaggar.(P.T)

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger