
Afisa
Uhusiano Airtel Tanzania Jane Matinde akiongea wakati wa kuchezesha droo
ya fainali za taifa ya michuano ya vijana chini ya umri 17 ya Airtel
Rising Stars. Kushoto ni Mkurungenzi wa maendeleo ya soka la wanawake
TFF Amina Karuma na katikati Mkurugenzi wa Ufundi TFF Salum Madadi.

Mkurungenzi
wa maendeleo ya soka la wanawake Tanzania Amina Karuma akiongea na
waandishi wa habari wakati wa kuchezesha droo ya michuano ya vijana
chini ya umri 17 ya Airtel Rising Stars ngazi ya taifa. Katikati ni
Mkurungenzi wa Ufundi TFF na kulia Afisa Uhusiano Airtel Tanzania Jana
Matinde.

Mkurungenzi
wa Ufundi TFF Salum Madadi akiongea na waandishi wa habari wakati wa
kuchezesha droo ya michuano ya vijana chini ya umri 17 ya Airtel Rising
Stars ngazi ya Taifa. Kushoto ni Mkurungenzi wa maendeleo ya soka la
wanawake Tanzania Amina Karuma.
TIMU za
soka za wasichana za Lindi na Arusha zimepangwa kukutana katika mechi ya
fungua dimba ya mashindano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya
Airtel Rising Statrs ngazi ya taifa katika uwanja wa Kumbukumbu ya
Karume, jijini Dar es Salaam, Jumanne, Septemba 6, 2016.
Mashindano
hayo yanayojumuisha timu za wasichana na wavulana yatafunguliwa rasmi
siku hiyo ya Jumanne mchana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa
Paul Makonda ambaye atashuhudia mechi ngumu ya wavulana kati ya Mwanza
na Ilala.
Timu
nyingine zinazoshiriki katika michuano hiyo yenye lengo la kuibua vipaji
ni Temeke, Kinondoni, Morogoro, Arusha, Mbeya, Lindi na Zanzibar.
Tayari timu zimeshawasili na kupiga kambi katika shule ya Filbert Bayi
iliyoko Kibaha.
Akizungumza
wakati wa hafla ya kupanga makundi iliyofanyika katika ofisi za
shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF), Mkurungenzi wa Ufundi Mwalimu
Salum Madadi alisema kuwa maandalizi yote ya mashindano hayo ngazi ya
taifa yamekamilika.
Hafla
hiyo pia ilihudhuriwa na mkurengenzi wa maendeleo ya soka la wanawake
nchini Bi Amina Karuma ambaye aliyaelezea mashindano ya Airtel Rising
Stars kuwa ni chemchem ya wanasoka chipukizi wasichana kwa wavulana.
“Mashindano
ya Airtel Rising Stars yametusaidia kupata wachezaji wenye vipaji vya
ajabu ambao wanaunda timu za Serengeti Boys na timu ya taifa ya wanawake
yaani Twiga Stars”, alisema na kuwashukuru Airtel Tanzania kwa
kuendelea kudhamini mashindano hayo.
Kwa
upande wake, Ofisa Uhusiano wa Airtel Tanzania Jane Matinde alisema kuwa
kampuni yake inajivunia kuweza kutoa mchango katika soka la Tanzania.
“Airtel Rising Stars imekuwa chanzo cha kutumainiwa kwa klabu na timu za
Taifa kupata vijana chipukizi wenye vipaji. Tunaona fahari kuweza
kupata fursa ya kudhamini soka nchini Tanzania“alisema Matinde.
Michuano
ya Airtel Rising Stars ngazi ya Taifa inatarajia kufikia tamati siku ya
Jumapili, Septemba 11, 2016 ambapo bingwa kwa upande wa wasichana na
wavulana watapatikana na kukanidhiwa vikombe vya ubingwa.
Vilevile TFF itatangaza wachezaji nyota kwa wasichana na wavulana wataochaguliwa kuunda timu ya Airtel Rising Stars mwaka 2016.(P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment