
Viongozi
wakuu wa mataifa ya Kusini-Masahriki mwa Asia ASEAN,wametakiwa
kushirikiana zaidi kukabiliana na vitisho vya ugaidi, mabadiliko ya
tabianchi na masuala yanayowagawa kama vile mgogoro wa bahari ya China
Kusini.
Akiufungua
rasmi mkutano huo, rais wa Laos Bounnhang Vorachit, amesema kuna haja
kwa wao kushirkiana kwa karibu kufuatilia matukio na kuendelea
kuimarisha ushirikiano wa mataifa ya jumuiya hiyo ya ASEAN na pia
kushirikiana na jumuiya ya kimataifa. Viongozi wa mataifa yanaounda
jumuiya ya mataifa ya kusini-Mshariki mwa Asia ASEAN, walikuwa
wanakutana mjini Vientiane kwa Mkutano wao wa kilele wa kila mwaka,
ambao umehudhuriwa pia na Rais wa Marekani Barack Obama kwa mara mwisho.
"Changamoto
mbalimbali za kiusalama zimetokea katika sehemu nyingi za dunia katika
muundo wa ugaidi na itikadi kali, majanga ya asili, mabadiliko ya
tabianchi, mgogoro wa wakimbizi, usafirishaji binaadamu kimagendo,
migogoro ya maeneo na migogoro ya kivita. Wakati huo huo, ingawa uchumi
wa dunia umefufuka taratibu, kasi ya ukuaji imeendelea kuwa ndogo na
tete, Kwa kuzingatia hayo yote, kuna haja kwetu kufuatilia matukio hayo
kwa karibu na kuendelea kuimarisha ushirikiana kati ya mataifa
waanachama wa ASEAN," alisema rais Vochit.
Wasiwasi kuhusu China
Kulingana
na muswada wa taarifa ambayo itatolewa bmwishoni mwa mkutano, viongozi
hao walitarajiwa kuelezea wasiwasi mkubwa kuhusiana na hatua za China
kufukia sehemu ya bahari ya China Kusini kwa ajili ya matumizi yake
mengine. Lakini katika kile kinachoonekana kama mapinduzi ya
kidiplomasia kwa China, viongozi hao hawakutarajiwa kuitaja rasmi hukumu
iliyotolewa mwezi Julai na mahakama ya kimataifa ya utatuzi wa
migogoro, kwamba China haikuwa na haki ya kisheria kudai umiliki wa
sehemu kubwa ya eneo hilo la bahari. China iliipinga huku hiyo na
kuitaja kuw ani batili.
Kabla ya
mkutano huo, Ufilipino iliona kuwa huenda China inajipanga kuanza ujenzi
mwingine katika bahari ya China Kusini, baada ya meli 10, zikiwemo nne
zinazoonekana kama mashua kubwa, zilizoonekana karibu na kisiwa cha
Huangyan. "Hili ni jambo la kutia wasiwasi kwa sababu ni kisiwa chetu",
waziri wa ulinzi Lorenzana aliwambia waandishi wa habari mjini
Vientinane, na kuongeza kuwa ikiwa China itafanikiwa kujenga majengo
kisiwani hapo watakuwa hawawezi tena kukirejesha.
Obama kuwarai viongozi ASEAN
Rais
Obama alitarajiwa kuibua shuala hilo na viongozi wa ASEAN na kujadili
haja ya kutatua mgogoro wa kieneeo chini cha sheria ya kimataifa kulinga
na taarifa iliyotolewa na ikulu ya White House. Pia alitarajiwa
kuwahakikishia viongozi wa kanda ya Kusini-Mashairki mwa Asia juu ya
dhamira ya Marekani kwa kanda hiyo wakati wa ziara yake nchini Laos, ya
kwanza kwa rais wa Marekania alieko madarakani.
Jumuiya
ya ASEAN yenye nchi wanachama 10 inazijumlisha nchi za Brunei,Cambodia,
Indonesia, Laos, Malaysia, Myanmar, Ufilipino, Singapore, Thailand na
Vietnam. Mkutano wa leo utafuatiwa na mikutano kadhaa mingine kesho
Jumatano, na mkutano wa kile siku ya Alhamisi kati ya viongozi kutoka
ASEAN an mataifa mengine yakiwemo Marekani, China, Urusi, India, Korea
Kusini, Japan, Australia na New Zealand. DW
SHARE
No comments:
Post a Comment