
Mgeni
Rasmi Mhe. Mahmoud Thabit Kombo, Waziri wa Afya, Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar (mwenye kaunda suti ya kijivu) akiwa katika Jukwaa Kuu na
viongozi waandamizi kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ),
Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na viongozi kutoka
Shirika la Idadi ya Watu Duniani (UNFPA). Wengine pamoja nae ni Bw.
Barnabas Yisa, Ofisa Mkaazi Mfawidhi UNFPA Tanzania (kushoto) na Mhe.
Issa Juma Ally, Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini B (kulia).

Mhe.
Salama Abuu Talib, Waziri wa Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira ambaye
pia ni Kaimu Waziri wa Wizara ya Fedha na Mipango, Zanzibar akihutubia
wananchi waliohudhuria sherehe hizo.

Wananchi
wa kijiji cha Kilombero, Wilaya ya Kaskazini B, Mkoa wa Kaskazini
Unguja wakifuatilia kwa makini yaliyokua yakijiri wakati hafla ya
uzinduzi wa taarifa hiyo.

Bw.
Barnabas Yisa, Ofisa Mkaazi Mfawidhi UNFPA (mwenye shati jeupe) akitoa
neno kwa wananchi walioshiriki shughuli ya uzinduzi wa Taarifa ya Hali
ya Idadi ya Watu Duniani. Kushoto ni Bibi. Christina Mwanukuzi Kwayu,
Mwakilishi Msaidizi, UNFPA akitafsiri kwa lugha ya kiswahili hotuba ya
Ofisa Mkaazi Mfawidhi.

Mhe.
Issa Juma Ally, Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini B, akitoa neno kwa wananchi
waliohudhuria uzinduzi wa Taarifa hiyo kabla ya kumkaribisha mgeni
rasmi ili aweze kuongea na wananchi na kuizindua rasmi.

Mgeni
Rasmi Mhe. Thabit Kombo, Waziri wa Afya, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar
akieleza juu ya fursa ndogo waliyonayo wasichana ya kumaliza skuli
kuliko wavulana na wako katika hatari zaidi ya kukabiliwa na ndoa za
utotoni, ajira za watoto, ukeketaji na matendo mengine ya udhalilishaji.

Mhe.
Thabit Kombo, Waziri wa Afya, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar akikata
utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Taarifa ya Hali ya Idadi ya Watu
Duniani.

Mgeni
Rasmi Mhe. Thabit Kombo, Waziri wa Afya, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar
akiwaonyesha wananchi kitabu cha Taarifa ya Hali ya Idadi ya Watu
Duniani mara baada ya kuizindua.
SHARE
No comments:
Post a Comment