KUFUATIA Uhaba wa madawati katika shule za msingi halmashari ya jiji la Tanga na wanafunzi kusomea chini, Kiwanda cha Saruji cha Simba Cement kimetoa madawati 100 kwa shule tatu.
Shule hizo ambazo zimefaidika na mpango huo ni Magaoni, Kiruku, Mkombozi na Martini Shamba zote za halmashauri ya jiji la Tanga.
Akizungumza wakati wa makabidhiano mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Tanga , Thobias Mwailapwa, Mkuu wa Idara Rasilimali watu kiwabda cha Saruji , Diana Malambusi amesema msaada huo umekuja baada ya kuona kero ya wanafunzi kusomea chini kutoisha.
Akizungumza
katika hafla fupi ya makabidhiano, Mkuu wa Wilaya, Thobias Mwailapwa,
amekishukuru kiwanda hicho (Simba Cement) na kuyataka mashirika na
taasisi pamoja na makampuni kuiga mfano huo ili kumaliza kero ya
wanafunzi kusomea chini.
Kwa upande wake Afisa elimu shule ya
msingi jiji , Khalifa Shemahonge, amesema madawati hayo yatatumika kama
inavyokusudiwa na kuahidi kuyatunza ili kuongeza uelewa wa wanafunzi
darasani.
Mkuu wa
Idara ya Rasilimali watu kiwanda cha Tanga Cement (Simba Cement), Dianna
Malambugi (kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Thobias
Mwailapwa, madawati 100 kwa shule tatu za msingi, Magaoni, Kiruku,
Mkombozi na Martin Shamba za halmashauri ya jiji la Tanga kupunguza
uhaba wa madawati na wanafunzi kusomea chini.
Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Thobias Mwailapwa, akimkabidhi Afisa Elimu Shule ya Msingi halmashauri ya jiji la Tanga, Khalifa Shemahonge madawati 100 kwa shule tatu ya, Magaoni, Kiruku, Mkombozi na Martin Shamba yaliyotolewa na kiwanda cha Saruji cha Simba Cementi kupunguza uhaba wa madawati kwa shule hizo.
Mkuu wa
Wilaya ya Tanga, Thobias Mwailapwa mwenye suti bluu (katikati) na Afisa
Elimu shule ya msingui halmashauri ya jiji la Tanga, Khalifa Shemahonge
(kulia) wakiwa na wafanyakazi wa kiwanda cha Simba Cement mara baada ya
makabidhiano ya madawati 100 kwa shule tatu za halmashauri ya jiji la
Tanga .
Walimu wa
shule za msingi Magaoni, Kiruku, Martin Shamba na Mkombozi wakiwa
katika picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Tanga na wafanyakazi wa
kiwanda cha Saruji cha Simba Cement mara baada ya makabidhiano ya
madawati 100 kwa shule hizo.
Habari hii ni kwa hisani ya blog ya kijamii ya tangakumekucha 0655 902929 (P.T)
Habari hii ni kwa hisani ya blog ya kijamii ya tangakumekucha 0655 902929 (P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment