
Wabunge
Viti Maalum Mkoa wa Pwani Zaynab Matitu Vullu na Subira Khamis Mgalu
wakikagua Ujenzi wa Daraja la Usimbe -Maparoni - Msala wilaya mpya ya
Kibiti.
...............................................................
Wabunge
Viti Maalum Mkoa wa Pwani Zaynab Matitu Vullu na Subira Khamis Mgalu
wamefanya Ziara ya Kukagua Ujenzi wa Daraja la Usimbe -Maparoni - Msala
lililopo Wilaya Mpya ya Kibiti na kukabidhi kiasi cha milioni moja
1.000.000/= huku shilingi milioni Nne na elfu Hamsini zikiwa zimeingizwa
kwenye akaunti na kufanya jumla ya fedha ya mchango walioutoa katika
ujenzi wa daraja hilo kufikia shilingi Milioni Tano na Elfu Hamsini
5.050.000/=.
Msaada
huu unafuatia Ahadi iliyotolewa na Wabunge hao wakati wa Kampeni katika
kusaidia Wananchi wa Maeneo ya vijiji hivyo ambao kwa sasa wanatumia
Daraja la Muda lililojengwa kwa miti na wananchi wenyewe ili kuwawezesha
Kuvuka mto .Ni muda mrefu sasa hawana daraja ambapo
kipindi cha mvua Maji hujaa na kuwapa shida wananchi hasa Kina Mama
Wajawazito na Wanafunzi hushindwa Kuvuka na baadhi yao wamepoteza Maisha
kwa kusombwa na maji kutokana na tatizo la kukosekana kwa Daraja hilo.
Bajeti
ya Ujenzi wa Daraja hilo imefika Milioni Kumi ambapo wabunge hao
wamewashukuru Wadau wote waliowaunga Mkono katika kutimiza Ahadi hii ya
kusaidia Wananchi wa Vijiji takriban saba hususan Kina Mama Wajawazito
na Wanafunzi ili kuvuka usalama wanapokwenda Kupata huduma mbalimbali
zikiwemo Afya na Elimu nk.
Wabunge
hao waliwaomba wadau mbalimbali walioahidi kuchangia ujenzi wa daraja
hilo katika Kata Mbili za Maparoni na Msala na Wilaya ya Mafia
kukamilisha ahadi zao mungu awajaalie wafanikiwe kupata chochote ili
waweze kuchangia ili tuweze kukamilisha ujenzi huo ambapo bado unahitaji
shilingi milioni 5.000.000 zingine ili kukamilisha bajeti ya ujenzi wa
daraja hilo ambayo ni shilingi milioni kumi 10,000.000.
"Tunaamini
mtakapo pata fursa Mtachangia Mwenyezi Mungu Awawezeshe Amiin" Alisema
Mh. Subila Mgalu huku akimaliza kwa kuwashukuru Viongozi wa Chama,
Jumuiya zake , Serikali Ngazi ya Wilaya na Kata kwa mashirikiano makubwa
na mapokezi Mazuri .
Daraja
litakapokamilika litasaidia Vijiji Saba Kipoka , Usimbe ,Maparoni
,Msala ,Twasalie ,Kihasi ,Kiechuru ,Kibanjo Kata Tatu na pia Njia hii
inatumiwa Kufika mpaka Mafia. ambapo kwa sasa kumekuwa na athari yingi
hasa kwa akina Mama wengi wajawazito wanashindwa kuvuka Maji yanapojaa
na kupelekea kujifungua Njiani.

Mbunge
Viti Maalum Mkoa wa Pwani Subira Khamis Mgalu akifurahia jambo wakati
wa Ziara ya Kukagua Ujenzi wa Daraja la Usimbe -Maparoni - Msala

Mbunge
Viti Maalum Mkoa wa Pwani Subira Khamis Mgalu wakionyeshwa vipimo vya
daraja na wananchi wakati wa Ziara ya Kukagua Ujenzi wa Daraja la Usimbe
-Maparoni - Msala

Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Pwani Zaynab Matitu Vullu akiwa amekaa na wakina mama wakati wa ziara hiyo wilaya mpya ya Kibiti

Wabunge
Viti Maalum Mkoa wa Pwani Zaynab Matitu Vullu na Subira Khamis Mgalu
wakikabidhi fedha taslimu shilingi milioni moja kwa kwa ajili ya Ujenzi
wa Daraja la Usimbe -Maparoni - Msala wilaya mpya ya Kibiti.

Hali
ya Vyombo vya Usafiri waliyoikuta wabunge hao wakati walipofanya ziara
Mwaka Jana 3/10/2015 ambayo iliwagusa na kuwahamasisha kutafuta Michango
ya ujenzi wa daraja hilo Daraja

Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Pwani Subira Khamis Mgalu akizungumza na wananchi wakati wa ziara hiyo.

Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Pwani Zaynab Matitu Vullu akizungumza na wananchi wakati wa ziara hiyo.
SHARE
No comments:
Post a Comment