Mkurugenzi
wa Taasisi ya Namaingo Business Agency (T) LTD, Ubwa Ibrahim
akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari pamoja na
wajasiriamali kuhusu jinsi ya kuzichangamkia fursa mbalimbali za
ujasiriamali katika Makao Makuu ya kampuni hiyo, Ukonga, Dar es Salaam
leo. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA-KAMANDA WA MATUKIO BLOG
Mkurugenzi
wa Taasisi ya Namaingo Business Agency (T) LTD, Ubwa Ibrahim
akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari pamoja na
wajasiriamali kuhusu jinsi ya kuzichangamkia fursa mbalimbali za
ujasiriamali katika Makao Makuu ya Taasisi hiyo, Ukonga, Dar es Salaam
jana.
Kushoto ni Mratibu wa Wanahabari wa kampuni hiyo, Jamila Abdalah.
Kushoto ni Mratibu wa Wanahabari wa kampuni hiyo, Jamila Abdalah.
Ubwa
akifafanua jambo wakati wa mkutano huo, ambapo aliwaomba wananhabari
kutumia kalamu zao kuwaelimisha wananchi kuhusu fursa hizo za
ijsiriamali ili waondokane na umasikini.
Baadhi ya wanahabari na wajasiriamali wakaiwa katika mkutano huo
KAMPUNI
ya Namaingo Business Agency (T) LTD, mwezi ujao inazindua mradi mkubwa
wa ufugaji kuku chotara wenye thamani ya sh. bilioni 30 utakaowawezesha
wananchi 3000 wa mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma.
Akizungumza
wakati wa mkutano na waandishi wa habari, Makao Makuu ya kampuni hiyo,
Ukonga, Dar es Salaam leo, Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Ubwa Ibrahim
amesema mradi huo mkubwa na wa aina yake umeanza kujengwa Lindi
Vijijini.
Amesema
kuwa watakaonufaika ni wananchi wa mikoa hiyo watakao timiza taratibu
zote, ambapo kila mmoja atakopeshwa na benki sh. mil. 10 ambazo
zitakwenda moja kwa moja kwenye mradi wa kuku utakaokuwa unaendeshwa na
watalaamu kutoka Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
Anasema
kuwa mradi mzima utasimamiwa na JKT kwa ushirikiano na Kampuni ya
Namaingo ambapo mfugaji atafaidika kwa kupata faida baada ya mauzo
yatakayokatwa gharama zote za mradi huo.
Katika
mradi huo kila mwanachama atajengewa banda la kufugia kuku chotara 1000
watakaofugwa kisasa na kwa utalaamu unaotakiwa ili kupata kuku wenye
ubora na kilo nyingi hivyo kuuzwa kwa bei nzuri.
Alitaja baadhi ya vigezo na taratibu anazotakiwa mwanachama kukamilisha kabla ya kupatiwa mkopo huo kuwa ni; Kwanza kuwa mwanachama wa Namaingo, kufungua akaunti katika benki za NMB, CRDB, pia kujiunga na NSSF, NHIF, PSPF, Bima ya Maisha, kusajili jina la biashara Brela.

Pia
mwanachama anatakiwa kuwa na Tin number, ajiunge Mfuko wa Uwekezaji wa
Pamoja (UTT-AMIS), awe na leseni ya biashara, cheti cha TDFA, cheti cha
GSI, cheti cha TBS bila kusahau kopi ya kitambulisho cha mpigakura,
leseni ya udereva au kitambulisho cha utaifa.
Pia Kampuni hiyo inatarajia kufungua miradi mbalimbali ya kilimo na ufugaji mikoani itakayowanufaisha wananchi wengi. (P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment