Naibu
Waziri Wa Afya ,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Hamis
Kigwangalla akikagua baadhi ya pombe kali katika moja ya duka
alilolikamata lililopo mwenge Dar es salaam wakati wa msako zidi ya
watengenezaji pombe kali ambazo ni feki unaoendelea nchini.
Naibu
Waziri Wa Afya ,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Hamis
Kigwangalla katikati akimuhoji muuza duka la pombe kali ambazo ni feki
lilopo Manzese Dar es salaam wakati wa msako zidi ya watengenezaji pombe
kali ambazo ni feki unaoendelea nchini.
Naibu
Waziri Wa Afya ,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Hamis
Kigwangalla wa kwanza kulia akiwa ameshika beseni lililojaa vizibo vya
konyagi katika kiwanda feki kilichokamatwa maeneo ya sinza Dar es salaam
wakati wa msako zidi ya watengenezaji pombe kali ambazo ni feki
unaoendelea nchini kushoto ni Afisa kutoka TFDA.
Baadhi ya
nyenzo za kutengenezea pombe kali ambazo ni feki aina ya konyagi katika
kiwanda feki kilichokamatwa maeneo ya sinza jijini Dar es salaam wakati
wa msako zidi ya watengenezaji pombe kali ambazo ni feki unaoendelea
nchini.
Baadhi ya
pombe kali aina ya konyagi na amarula ambazo ni feki zilizokamatwa
katika duka la kuuza pombe kali lililopo manzese jijini Dar es salaam
wakati wa msako zidi ya watengenezaji pombe kali ambazo ni feki
unaoendelea nchini.
Baadhi ya
pombe kali aina ya konyagi na amarula ambazo ni feki zilizokamatwa
katika duka la kuuza pombe kali lililopo manzese jijini Dar es salaam
wakati wa msako zidi ya watengenezaji pombe kali ambazo ni feki
unaoendelea nchini.
Na Ally Daud-MAELEZO
Naibu
Waziri Wa Afya ,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Hamis
Kigwangalla ameongoza kikosi kazi katika msako wa Viwanda
vinavyotengeneza pombe Kali feki ikiwemo viroba na zinginezo na
kufanikiwa kukamata kiwanda feki kilichopo maeneo ya sinza jijini Dar
es salaam.
Akiingoza
msako huo Naibu Waziri Wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na
Watoto Dkt. Hamis Kigwangalla amesema kuwa msako huo unaofanywa na
Wizara hiyo inashirikiana na Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA
umefanikiwa kukamata kiwanda feki kinachotengeneza pombe aina ya viroba,
konyagi, Smirnoff na zedi kilichopo sinza jijini Dar es salaam.
“Tunafanya
msako huu kwa kushirikiana na kikosi kazi cha Serikali ili kuondoa
pombe haramu zinazotengenezwa kiholela na kwa kutozingatia viwango vya
ubora kwa maendeleo na Afya ya watanzania” alisema Dkt. Kigwangalla.
Aidha
Dkt. Kigwangalla ameongeza kuwa katika msako huo wamefanikiwa kukamata
kiwanda hicho kikiwa na nyenzo za kutengenezea pombe haramu kama vile
chupa za konyagi, vifuniko, lebo, vifuko na nyenzo zingine za
kutengenezea pombe hiyo haramu.
Dkt.
Kigwangalla amesema kuwa msako huo umebaini kwamba watengenezaji hao
wanatumia gongo na spiriti kutengeneza pombe kali kitu ambacho ni hatari
kwa afya ya watanzania hususani vijana hivyo kufanya nguvu ya taifa
kupotea.
Katika
msako huo pia ulifanikiwa kukamata maduka yanayouza pombe hizo maeneo
ya Mwenge na Manzese jijini Dar es salaam ikiwa chini ya msambazaji Bw.
Yusuf Yusuf Abdul Kalambo mkazi wa Kimara ambaye anatafutwa na jeshi la
polisi kwa ajili ya upelelezi zaidi.
Aidha
Dkt. Kigwangalla ameamuru wauzaji wa maduka hayo wafunge maduka yao mara
moja na kushikiriwa na Polisi mpaka pale upelelezi utakapokamilika ili
sheria stahiki ifuate mkondo wake aidha kulipa faini au kufutiwa leseni
za biashara.
Zoezi
hilo la kusaka Viwanda feki vinavyotengeneza pombe kali linafanywa na
Wizara ya Afya kwa kushirikiana na TFDA pamoja na jeshi la polisi ni
endelevu mpaka bidhaa feki zitapotoweka nchini.(P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment