Serikali ya Japan, imeidhinisha mpango wa kumruhusu mfalme Akihito wa nchi hiyo, ajiuzulu.
Mwaka jana mfalme huyo mwenye umri wa miaka 83, alielezea azma yake ya kuachia mamlaka kwa sababu za kiafya.
Amekuwa utawalani tangu mwaka 1989.
Iwapo hatua hiyo itaidhinishwa na kufaulu, atarithiwa na mwanawe Prince Naruhito.
Taarifa zasema kuwa atakabidhiwa mamlaka mwaka ujao wa 2018.
CHANZO: BBC
SHARE
No comments:
Post a Comment