Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limezitaka serikali ya Syria na
wapinzani kushiriki kwa nia moja bila ya masharti katika duru ijayo ya
mazungumzo ya kutafuta amani yatakayofanyika mjini Geneva tarehe 23
mwezi huu. Baraza la Usalama limetoa mwito kwa pande zote mbili
kutekeleza makubaliano ya kusimamisha mapigano yaliyofikiwa mwezi
Desemba mwaka uliopita. Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa pia
limezitaka nchi zinazounga mkono pande hizo mbili katika mgogoro wa
Syria zitumie ushawishi wao kukomesha ukiukaji wa makubaliano hayo aidha
kupunguza mapigano, kujenga hali ya kuaminiana na kuhakikisha kwamba
misaada inawafikia walengwa. Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa
Mataifa waliwaambia waandishi wa habari kwamba wanaziunga mkono juhudi
za mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa Staffan de Mistura
anayeushughulikia mgogoro wa Syria katika kutafuta suluhisho kuambatana
na makubaliano yaliyofikiwa mwaka 2012 mjini Geneva.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment