TRA

TRA

Wednesday, November 30, 2016

ESRF YAFANIKISHA MKUTANO WA 5 WA MWAKA, WAJADILI UCHUMI

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !



Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dr. Ashatu Kijaji akihutubia katika mkutano wa tano wa mwaka wa ESRF wa kujadili sera za jamii na mahusiano yake kwenye mabadiliko ya kiuchumi nchini Tanzania ulioandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF) jijini Dar es Salaam.(Picha na Said Khalfan wa KVS Blog)
"Serikali inapofanya mipango inatakiwa kupanga mipango ambayo inajaribu kujibu kero za mwananchi, kama ni elimu, kama ni afyaa au kama ni kilimo cha kisasa, tunapotengeneza sera tuwe tunauwianisha, hizo sera zikitekelezeka na mteja wa bidhaa awe ameandaliwa ili mkulima asiwe amepoteza nguvu bure," alisema Luhanjo na kuongeza.
"Tunazungumzia nchi ya viwanda, viwanda gani? na nchi yetu niya kilimo kwahiyo tunatarajia viwanda vingi vitakuwa ni vya kilimo, kwahiyo tunataraji mkulima mdogo aimalishwe ili aweze kuzalisha mazao yanayokwenda kiwandani ni lazima sera ziwe na uwiano mzuri."
Nae Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji alisema Serikali inafahamu kuwa nchi haiwezi kupiga hatua bila kuhusisha mwananchi mmoja mmoja na inachofanya kwa sasa na kuwashawishi watu wenye viwanda kutumia malighafi ambazo zinazalishwa nchini ili wakulima nchini wafaidike na uwepo wa viwanda nchini.
"Tunaamini hatuwezi kuwa na uchumi unaokua kama hali ya kijamii ya wananchi haikui na hata Rais Magufuli alikuwa akisema tangu akiwa katika kampeni kwamba Tanzania ya Magufuli niya viwanda, na viwanda hivi ni kwa ajili ya watu wetu,

Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini wa ESRF, Philemon Luhanjo, akizungumza katika mkutano wa tano wa mwaka wa kujadili sera za jamii na mahusiano yake kwenye mabadiliko ya kiuchumi nchini Tanzania ulioandaliwa na ESRF.
"Kwenye mpango wetu wa miaka mitano tumesisitiza maendeleo ya viwanda lakini vinavyotumia malighafi zinazozalishwa hapa nchini katika kilimo chetu, kwahiyo hatuwezi kuwa na viwanda kama kilimo hakijaendelea, hatuwezi kuwa maendelo ya kijamii kama kilimo chetu hakijaendelea, kilimo ndiyo uti wa mgongo wa taifa letu, kwahiyo tumejadili hilo ili kuona wananchi wetu wananufaika vipi," alisema Kijaji.
Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dk. Tausi Kida alizungumza kuhusu mkutano huo ambao umedhaminiwa na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) na kusema,"ESRF kwasasa hivi tupo kwenye mchakato wa kutengeneza Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu ya mwaka 2017, "Katika hiyo ripoti tumeweza kutaharisha ripoti 11 ambazo zitachangia katika utayarishishaji wa hiyo ripoti na dhumuni kubwa ni kuweza kuzijadili hizo ripoti na kupata uelewa mpana ni kwa kiasi gani sera za kijamii zina mchango mkubwa katika kuleta mageuzi ya kiuchumi hapa Tanzania."

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Tausi Kida akitoa maelezo kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi katika mkutano huo.

Mkuu wa Programu, Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP, Amon Manyama akizungumza katika mkutano wa tano wa mwaka wa kujadili sera za jamii na mahusiano yake kwenye mabadiliko ya kiuchumi nchini Tanzania.(P.T)

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger