Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika
la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez akimkabidhi
Ripoti ya Umoja wa Mataifa ya mpango wa misaada ya maendeleo UNDAP II
2016-2021 Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ruaha (RUCU) Iringa, Dr. Cephas Mgimwa
alipomtembelea ofisini kwake mjini Iringa.
UMOJA wa
Ulaya (EU) na Umoja wa Mataifa (UN) wameweka nguvu ya pamoja kuendesha
kampeni ya uelewa wa malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) nchini
Tanzania. Wakiwa Mkoani Iringa wamepata nafasi ya kuzungumza na wanachuo
1,000 kutoka vyuo vikuu vya Iringa na Ruaha kwenye semina iliyoelezea
malengo ya dunia ambayo ni sehemu ya ajenda 2030 ya maendeleo endelevu
duniani ambapo kati ya hao, vijana 50 wamepata semina ya mwongozo wa
kuwa mabalozi wa malengo hayo (Global Goals Champions).
Kampeni
hiyo imelenga kuwafanya vijana waelewe malengo 17 ya dunia ambayo kwa
sasa yana mwaka mmoja tangu yapitishwe na kuwatanabaisha wajibu wao
katika kufanikisha utekelezaji wake ndani ya mazingira ya Tanzania.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika
la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez akifafanua
jambo juu ya ripoti ya Umoja wa Mataifa ya Mpango wa misaada ya
Maendeleo 2016-2021 (UNDAP II) kwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ruaha (RUCU)
Iringa, Dr. Cephas Mgimwa alipomtembelea ofisini kwake mjini Iringa
Mwanasheria
wa Chuo Kikuu cha Ruaha Iringa, Martin Noel akiwa ameongozana Mtaalam
wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa nchini, Hoyce Temu kuelekea kwenye
ukumbi wa mikutano chuoni hapo sambamba Mratibu Mkazi wa Mashirika ya
Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja
wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez aliyeambatana na Mwakilishi wa Umoja
wa Ulaya (EU) nchini ambaye pia ni Afisa Miradi, Anna Muro.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika
la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez akiendesha
semina ya malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) kwa vijana 50 kutoka Chuo
Kikuu cha Iringa na Ruaha ambao watakuwa ni mabalozi wa malengo hayo ya
dunia huku lengo la UN ni kuwaelimisha vijana zaidi ya 30,000 ifikapo
mwaka ujao kuhusu malengo hayo ya dunia.
Mwakilishi
wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini ambaye pia ni Afisa Miradi, Anna Muro
akielezea fursa za ufadhili wa masomo nje ya nchi katika tovuti ya Umoja
wa Ulaya Tanzania wakati wa semina ya malengo ya maendeleo endelevu
(SDGs) kwa vijana 50 kutoka Chuo Kikuu cha Iringa na Ruaha ambao
watakuwa ni mabalozi wa malengo hayo ya dunia (Global Goals Champions)
huku lengo la UN ni kuwaelimisha vijana zaidi ya 30,000 ifikapo mwaka
ujao kuhusu malengo hayo ya dunia iliyofadhiliwa na EU.(P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment