Naibu
waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani akitoa
maelekezo kwa Meneja wa Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA), mkoa wa Mbeya Bw.
Issa Hamadi alipokagua uwanja wa ndege wa Songwe Mkoani Mbeya.
Naibu
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (wa pili
kushoto), akikagua na kupata maelezo ya njia ya kuruka na kutua ndege
katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Songwe Mkoani Mbeya, kulia kwa
waziri ni Kaimu Meneja wa uwanja huo Bw. Amir Hamis.
Naibu
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (mwenye
miwani) akikagua kifaa cha kupima kiasi cha jua katika Uwanja wa Ndege
wa Kimataifa wa Songwe Mkoani Mbeya.
Naibu
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani akitoa
maelekezo kwa mkandarasi DB Shapriya anayejenga jengo la abiria katika
uwanja wa ndege wa kimataifa wa Songwe Mkoani Mbeya.
Naibu
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani akikagua
daraja katika reli ya TAZARA mkoani Mbeya na kusisitiza uboreshwaji wa
haraka wa mazingira katika nguzo za daraja hilo ili kutoathiri daraja
hilo na reli kwa ujumla.
Naibu
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani akikagua
mashine aina ya (traction motor), inayotumika kuendeshea injini ya gari
moshi alipokagua karakana ya utengenezaji wa vichwa vya treni ya TAZARA
Mkoani Mbeya.
Mkuu
wa Mkoa wa Mbeya Bw. Amosi Makalla akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani walipokutana
kutathimini ziara ya Naibu Waziri huyo mkoani Mbeya.
…………………………………………………………………..
Viongozi
na wafanyakazi wa taasisi za Serikali wametakiwa kubadilika kimtazamo
ili kwenda sambamba na malengo na matarajio ya Serikali ya awamu ya tano
katika kukuza uchumi wa viwanda na kuongeza ajira.
Naibu
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani amesema
Serikali imedhamiria kufufua na kuyawezesha mashirika yake yote kufanya
biashara na kuzalisha faida ili kujitegemea na kuachana na utegemezi wa
ruzuku toka Serikalini.
Akizungumza
katika majumuisho ya ziara yake ya siku tatu mkoani Mbeya Eng. Ngonyani
amezitaka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA), Shirika la Reli la
Tanzania na Zambia (TAZARA), na Wakala wa Ufundi na Umeme nchini
(TEMESA) kubuni vyanzo vya mapato.
“Fanyeni
kazi kwa ubunifu ili mzalishe faida na kuwa na uwezo wa kujiongezea
mishahara na stahili mbalimbali, acheni kulalamika na kutegemea ruzuku
ya Serikali katika kila jambo”. Amesisitiza Eng. Ngonyani.
Amewataka
TAA kuhakikisha ndege nyingi zinautumia uwanja wa ndege wa kimataifa wa
Songwe kwani ukitumika vizuri unaweza kuwa kitovu cha uchumi kwa ukanda
wa kusini na nchi jirani kutokana na ubora wake.
Naibu
Waziri huyo amezungumzia umuhimu wa TAZARA kutafuta soko la ndani badala
ya kutegemea soko la nje pekee kwani kufanya hivyo kutapunguza mizigo
mingi inayosafirishwa kwa njia ya barabara na kuhamia kwenye reli hali
itakayopunguza msongamano na uharibifu wa barabara.
Ameziagiza
taasisi zilizo chini ya Wizara ya ujenzi kuiamini TEMESA, kufanya kazi
na taasisi hiyo na kulipa madeni zinazodaiwa ili kuiwezesha kukua na
kuaminika kwa taasisi nyingine na sekta binafsi.
Akizungumza
kwa niaba ya taasisi zilizo chini ya Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na
Mawasiliano Mwenyekiti wa taasisi hizo Eng. Paul Lyakurwa amesema
taasisi hizo zimejipanga kuboresha miundombinu ya reli, barabara na
mawasiliano ya simu na anga ili kufungua mikoa ya nyanda za juu kusini
na sehemu nyinginze za nchi na hivyo kuwezesha usafirishaji wa mazao na
bidhaa zilinazozalishwa katika mikoa hiyo kufika sokoni kwa wakati.
Naibu
waziria Ngonyani amekuwa katika ziara ya siku tatu Mkoani Mbeya ambapo
pamoja na mambo mengine amekagua meli mbili za mizigo zinazojengwa
katika Ziwa Nyasa, miradi ya barabara katika Wilaya ya Kyela, Busokelo
na Rungwe na kukagua uwanja wa ndege wa kimataifa wa Songwe na Karakana
ya kutengeneza vichwa vya treni ya TAZARA.
SHARE
No comments:
Post a Comment