Mfuko
wa Taifa wa Bima ya Afya NHIF kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo
ya UJERUMANI, wamezindua mradi wa huduma za matibabu kwa wanawake
wajawazito katika mikoa ya Mtwara na Lindi, unaojulikana kama Mradi wa
Tumaini la Mama.
Akuzungumza
katika uzinduzi huo, Waziri wa Afya Mh. Ummy Mwalimu amewahimiza
wanaume kushiriki kikamilufu kwa kuwapeleka wake zao Kliniki na kupata
maelekezo kwa pamoja juu ya matunzo ya ujauzito.
Aidha
amewataka wakazi wa mikoa ya Lindi na Mtwara kuzingatia uzazi wa mpango
na kuwapunguza watoto wa kike kwenda shule, badala ya kuwaona mapema
Ummy
amesema Mradi huo unalenga kuwahuduma wanawake wanatoka katika kaya
masikini ambazo zimekuwa zikilazimika kutumia njia zisizo salama za
kujufungua kutokana na kukosa fedha za kugharamia huduma hizo katika
vituo vya matibabu.
Kupitia
mradi huo Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya utawalipia huduma za matibabu
wanawake wajawazito wote wa mkoa ya Mtwara na Lindi baada ya
kujiandikisha kwenye vituo vya matibabu vilivyosajiliwa karibu nao.
Mradi
wa Tumaini la mama pia utawapa kadi Mfuko wa Afya ya Jamii CHF wanawake
watakaojifungua chini ya mradi huo pamoja na kaya zao.
Mradi
huo ulioanza kutekelezwa ktk mikoa ya Mbeya na Tanga tangu mwaka 2012,
umekuwa na mafanikio makubwa ambapo hadi sasa zaidi ya wanawake Laki
mbili wamenufaika nao.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu
akizungumza katika uzinduzi wa mradi wa huduma za matibabu kwa wanawake
wajawazito katika mikoa ya Mtwara na Lindi, unaojulikana kama Mradi wa
Tumaini la Mama mkoani Mtwara.
Mkuu
wa Mkoa wa Mtwara Halima Dendego akizungumza na wananchi waliojitokeza
kwa wingi kwenye uzinduzi wa mradi wa huduma za matibabu kwa wanawake
wajawazito katika mikoa ya Mtwara na Lindi, unaojulikana kama Mradi wa
Tumaini la Mama mkoani Mtwara.
Mwakilishi
wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Dkt.
Aifena Mramba akitoa maelezo mafupi ya Mradi wa Tumaini la Mama mkoani
Mtwara.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu
(katikati) kwa kushirikina na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Halima Dendego
(kulia) na Mwakilishi Ubalozi wa Ujerumani,Julia Hannig (kushoto) kukata
utepe kuzindua rasmi Mradi wa Tumaini la Mama.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu
akimkabidhi Mayasa Maunda vifaa vya kujifungulia katika uzinduzi wa
Tumaini la Mama
Mwimbaji wa muziki wa taarab, Isha Mashauzi akitumbiza kwenye kuzindua rasmi Mradi wa Tumaini la Mama mkoani Mtwara.
Baadhi kina mama waliokabidhiwa vifaa vya kujifungulia wakiwa katika picha ya pamoja katika uzinduzi wa Tumaini la Mama
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu akiwa
katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wakiwemo wa mikoa ya
Mtwara na Lindi.
Baadhi wa viongozi waliogika kwenye uzinduzi wa Tumaini la Mama mkoani Mtwara.
SHARE
No comments:
Post a Comment