Mwandishi Wetu
MKURUGENZI
wa Mamlaka ya usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Deusdedit Kakoko amesema
hataki kusikia dawa za kulevya zimepita katika bandari hiyo.
Mbali
na dawa hizo, amesema hataki kuona nyara za Serikali, silaha haramu, bidhaa za mionzi
na nyingine zisizofaaa zikipitishwa katika bandari.
Kakoko
alitoa kauli hiyo wakati akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo ya siku tano ambayo
yalifanyika jana jijini Dar es Salaam.
Mafunzo
hayo yalitolewa kwa watumishi zaidi ya 20 wa TPA na Mamlaka ya Mapato Tanzania
(TRA) kutoka Dar es Salaam na Tanga
Kakoko
alisema anaamini kupitia mafunzo hayo watumishi hao watabadilika na kwenda kwa
wakati uliopo.
Alisema
mafunzo hayo yana lengo la kuwajengea
uwezo wafanyakazi wa mamlaka hizo kutumia mashine za kukagua mizigo kwa
teknolojia
Kakoko alisema iwapo watumishi hao watatumia
siku tano hizo ipasavyo ni dhahiri kuwa wataonmgeza usimamizi katika bandari
zotec mbili.
“Naipongeza
Serikali ya Tanzania na Serikali ya Watu wa China kwa kuwezesha mradi huu
kukamilika. Tunatarajia mafunzo hayo yatawaongeza uwezo wa wafanyakazi, ufanisi
wa bandari pamoja na kuongeza mapato ya Serikali,” alisema.
Kakoko
aliwaagiza washiriki wa mafunzo kuhakikisha kuwa watakapokuwa wanafanya kazi
katika mashine hizo wahakikishe wanafanya tathmini ya mizigo inayoonekana
katika kontena kama ina taarifa sahihi kwa kulinganisha na nyaraka za kuagizia
mizigo husika.
Mkurugenzi
aliwataka waashiriki hao kuhakikisha wanajifunza kufanya matengezo ya mashine
hizo angalau kwa asilimia 50 kuliko kutegemea wataalamu kutoka nje pekee.
Mhandisi
Kakoko alisema TPA kwa kushirikiana na TRA watahakikisha waendesha scanners
wanajifunza kufanya matengezo kwa asilimia mia moja (100) ili kuondokana na
gharama za kutumia wataalam kutoka nje.
Wakandarasi
kutoka Kampuni ya Nuctech Limited ndio wanaendesha mafunzo hayo baada ya
kukamilisha mradi wa ufungaji wa Scanner katika Bandari ya Dar es Salaam na
Tanga.
Meneja
Mradi Zhang Sheng alisema mradi umekamilika na sasa wako katika hatua ya pili
ya mafunzo na scanner hiyo mpya inaweza kutumika muda wowote mara baada ya
kukamilisha mafunzo.
Kwa
mujibu wa meneja huyo scanner hiyo inauwezo wa kusoma na kupeleka taarifa na
picha za mizigo mubashara (live) kwenye mifumo ya TPA na TRA kwa wakati mmoja
bila kuchelewa.
Kukamilika
kwa mradi huo kunatokana na maagizo ya Rais wa Dk. John Magufuli kuwa TPA na
TRA zishirikiane kuendesha mashine za kukagua mizigo zinazotoa taarifa na picha
mubashara, pamoja na kufanya kazi pamoja ili kuhakikisha Serikali haipotezi
mapato na kupitisha mizigo haramu.
SHARE
No comments:
Post a Comment